.
.
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume Kizigo amewataka wahitimu wa mafunzo ya asklari wa akiba katika kijiji cha Limamu wilayani humo kuilinda amani ya nchi yetu kwa kutoa taarifa dhidi ya wahalifu au kuwakamata wahalifu wenye nia mbaya na amani ya nchi yetu.
Kizigo aliwataka kuwa askari wema wenye kufuata sheria za kazi zao katika kuisaidia serikali huku akiwataka pia wasijiingize katika kupokea rushwa katika kazi zao kwa kuwa rushwa ni adui Wa haki katika jamii.
“Tunawategemea katika kuwakamata waweka mimba wanafunzi , hivyo mkijihusisha na upokeaji rushwa mtasababisha kutowakamata wahalifu na nafasi ya kazi yako haitakuwa na manufaa kwa jamii na hata kwa serikali “ alisema Kizigo.
Ofisa mtendaji wa kijiji cha Limamu bi. Agnes Nchimbi alisema kuwa vijana waliojiandikisha katika kujifunza Mgambo walikuwa 140 lakini kutokana na sababu zisizozuilika za kiafya vijana wengine waliacha na kubakiwa na vijana 91 ndio waliohitimu mafunzo hayo katika kijiji chake.
Pancras Newa mhitimu wa mafunzo hayo alisema walianza mafunzo mwezi mei 2020 na kuhitimu mwezi januari 2021 hivyo aliiomba serikali kuendelea kutoa mafunzo kwa vijana wengine kwa kuwa mafunzo hayo yanawafanya vijana wawe wakakamaVu , kuzijua mbinu mbalimbali za kivita pamoja na kujua kutumia silaha alisema Newa.
Naye mwenyekiti wa kijiji cha Limamu bwana Magnus Ndunguru alisema walihamasisha vijana kujiunga na Mgambo katika kijiji hicho kupitia mikutano ya hadhara ya kijiji na kuwapata vijana 140 lakini kulingana na matatizo ya kiafya walibahatika kuhitimu ni hao 91.
Sherehe ya kuhitimu mafunzo ya jeshi la akiba katika kijiji cha limamu yalifanyika katika uwanja wa shule ya msingi Tumaini ambapo mkuu wa wilaya ya Namtumbo alipokea viapo vya askari wa akiba hao pamoja na kukagua gwaride lililoandaliwa na askari hao wa akib
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: S.L.P 55 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0765142640
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2018Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.