Mbunge wa Namtumbo Vitta Kawawa aliupongeza uongozi wa SONAMCU uliomaliza muda wake kwa kuanzisha kiwanda cha vifungashio wilayani Namtumbo ili kuondoa adha vya kuagiza vifungashio kutoka nje ya wilaya.
Kawawa aliyasema hayo kwenye mkutano mkuu wa wanachama uliofanyika katika ukumbi wa SONAMCU katika manispaaa ya Songea ambapo pamoja na mambo mengine kiwanda hicho alisema kitawawezesha wana Namtumbo kupata ajira .
“Nilipita mwenyewe kuangalia ujenzi wa kiwanda hicho na nikaulizia kama ujenzi huo unafanywa kwa hela za mkopo, nikaambiwa kuwa wanajenga kiwanda hicho kwa kutumia mapato ya ndani ya chama hicho na sio mkopo , nimefurahishwa sana na uongozi huo” alisema kawawa.
Pamoja na hayo Kawawa aliwataka wanachama Kutumia mkutano huo kuchagua viongozi wenye moyo wa kuendeleza SONAMCU ili kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli na kuacha ubabaishaji ,wizi ,ubadirifu wa fedha za wanaushirika na wawachague viongozi waadilifu .wachapa kazi na waaminifu.
Naye mwenyekiti aliyemaliza muda wake bwana Salumu Brashi katika mkutano huo aliwaomba wanachama kuwa waangalifu katika kuchagua , wawe makini katika kuchagua viongozi kwa kuwa uongozi ni dhamana ya kutumikia wanachama na sio faida ya mtu na familia yake.
Mwenyekiti mpya wa SONAMCU Bwana ALLY Haji Chemka kutoka chama cha msingi Mgombasi wilayani Namtumbo alikuwa mgombea pekee katika kiti cha uenyekiti katika mkutano huo alidai atasimamia vyema chama kikuu cha ushirika SONAMCU Ili kifikie malengo yaliyojiwekea .
Wengine waliochaguliwa katika mkutano huo ni makamu mwenyekiti bwana Bwana Grasiani Nyoni ,Haji Hashimu Haule,Hamisi Isime,Abu Nihamba,Mohamedi Kimilamata na Hamisi Luoga hao katika nafasi ya ujumbe wa bodi.
MWISHO.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: S.L.P 55 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0765142640
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2018Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.