Wilaya ya Namtumbo ni mojawapo ya wilaya zilizopo tanzania ambazo asilimia tisini ya uchumi wake inategemea Kilimo. Fursa kubwa iliyopo Wilayani Namtumbo ni Biashara ya Mazao kiasi ambacho husababisha wafanyabiashara mbalimbali kufika na kununua mazao na kuyasafirisha nje na ndani ya Mkoa wa Ruvuma kwaajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo matumizi ya Binadamu, uzalishaji wa bidhaa za viwandani na vyakula vya wanyama.
Mazao yanayolimwa wilayani namtumbo ni pamoja na;
Mpunga, Mahindi, Mbaazi, Karanga, Alizeti, Viazi, Mihogo, Tumbaku, Maharage, Kahawa, Ufuta, Nazi, Korosho na Ndizi
Kilimo ndio Shughuli kuu ya Uchumi wa Wilaya ya Namtumbo, ambayo ndiyo iliyoajiri asilimia 95% ya wakazi wote wa Namtumbo, Ikiwa eneo lote la wilaya ni kilometa za mraba 20,375 kati yake kilometa za mraba 600 ni eneo la kilimo.
Zao la Korosho linalolimwa Wilayani Namtumbo
Zao la Mpunga linalolimwa Wilayani Namtumbo
Zao la Mahindi linalolimwa Wilayani Namtumbo
Zao la Ufuta linalolimwa Wilayani Namtumbo
Zao la Karanga linalolimwa Wilayani Namtumbo
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.