• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Complaints |
    • Gms |
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu ya Halmashauri
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji/Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Mipango, Uchumi na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Utumishi na Utawala
      • Maji
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • TASAF
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Fursa za Kilimo
    • Fursa za ufugaji
    • Fursa za Madini
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokalika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo za Halmashauri
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
    • Taarifa
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma/Vyombo Mbalimbali vya Habari
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali

BARAZA LA USHAURI RUVUMA KUUNDA TUME KUSUASUA MIRADI YA REA

Tarehe ya Kuweka: January 3rd, 2022


Kikao cha baraza la ushauri  Mkoa wa Ruvuma kilifikia maamuzi ya kuunda tume kufuatilia mienendo ya makampuni  yanayotekeleza miradi ya umeme vijijini  REA kusuasua  katika utekelezaji wake hali inayoleta  kero kwa wananchi  katika mkoa wa Ruvuma .

Wakiongea  katika kikao hicho mbunge wa  Tunduru  kusini Daimu Mpakate alimwomba mkuu wa mkoa wa Ruvuma kuwaita wakandarasi  wanaosimamia utekelezaji wa umeme vijijini  REA kujiridhisha na sababu inayosababisha kusuasua kwa utekelezaji wa miradi ya umeme vijiji katika mkoa wa Ruvuma .

Mbunge wa madaba Joseph Mhagama  kwa upande wake alidai maamuzi  magumu ya kuwakataa wakandarasi  wanaochelewesha  utekelezaji  wa miradi unahitajika kwani bila kufanya hivyo  utekelezaji wa miradi  haufanyiki  kwa wakati .

Mhagama  alitolea mfano wa mkandarasi  aliyekuwa anasimamia mradi wa maji jimboni kwake kuwa walichukua maamuzi magumu  ya kumsimamisha  na mkandarasi  aliyepewa  yupo saiti  anachapa  kazi hali iliyoondoa malalamiko kwa wananchi  kwa kuwa wananchi kwa sasa wanamwona mkandarasi  hatua kwa hatua kazi anazozifanya  na kuondoa malalamiko tofauti na yule aliyesimamishwa  na kushauri  baraza kuchukua maamuzi magumu ya kuwasimamisha wakandarasi wanaokwamisha miradi ya umeme vijiji  REA.

Juma  Pandu  mwenyekiti  wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo alikiomba kikao hicho kutafuta mbinu mbadala ya kuwafanya  wakandarasi  hao wafanye kazi zao kwa haraka badala ya kuvunja  mkataba kwa kuwa watawasababishia  hasara  kubwa wakandarasi hao lakini pia itachukua muda mrefu tena wa mchakato wa kuwapata wakandarasi wengine na wakati mwingine kupelekana mahakamani .

Mhandisi  Stella Manyanya Mbunge  wa Nyasa  alishauri kabla ya kuvunja mkataba kikao kinatakiwa kijiridhishe sababu ya wakandarasi wa miradi ya umeme vijijini REA wanakumbana na changamoto ipi ambayo inaweza kuwa ndiyo inayosababisha miradi kuchelewa na changamoto hizo zinaweza zikawa sio za mkandarasi ni za mwenye kutoa kazi  hivyo inatakiwa kulishughulikia  jambo hilo kwa busara kubwa alisema Manyanya.

Mwenyekiti  wa chama cha Mapinduzi  mkoa wa Ruvuma  Oddo  Kirian Mwisho pamoja na mambo mengine aliwaambia wajumbe wa baraza la ushauri la mkoa kuwa chama kilimwomba mkuu wa mkoa kuwaita wakandarasi  wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini  REA baada ya kamati ya siasa mkoa kupita katika wilaya kufuatilia utekelezaji  wa ilani na kukumbana na malalamiko makubwa kutoka kwa wananchi kuhusu kusuasua kwa miradi ya umeme vijiji REA.

Mwisho alidai wakati wa kikao cha mkuu wa mkoa na wakandarasi hao hakuna mkandarasi  aliyedai anashindwa  kutekeleza  mradi kwa sababu anadai fedha, zaidi ya kuhaidi kufanya kazi kwa kuongeza kasi zaidi lakini hali bado ni ileile alisema mwenyekiti wa chama mkoa Oddo Mwisho.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Generali (Balozi) Wilbert Ibuge baada ya kupokea maombi na ushauri wa wajumbe kuhusu azimio la  kuunda tume ya kuchunguza sababu ya kusuasua kwa miradi ya umeme vijiji Rea aliridhia azimio la kuunda tume itakayofanya ufatiliaji na kutoa mapendekezo kwake kabla ya tarehe 20 mwezi  machi 2022.

Kikao cha baraza la ushauri la mkoa wa Ruvuma kilifanyika jana katika ukumbi  wa manispaa ya songea kilichotanguliwa na maombi ya mvua na kisha kujadili mambo ya maendeleo yanayohusu mkoa wa Ruvuma na Taifa kwa ujumla.

Mwisho.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WAOMBAJI WA KAZI YA MUDA YA SENSA WALIOFAULU USAILI NA KUITWA KWENYE MAFUNZO July 27, 2022
  • TAARIFA KWA UMMA June 27, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WAOMBAJI WA KAZI YA MUDA YA SENSA WALIOFAULU USAILI NA KUITWA KWENYE MAFUNZO July 27, 2022
  • MABADILIKO YA TAREHE YA KUFANYA USAILI June 22, 2022
  • Ona zote

Habari Mpya

  • ORODHA YA MAJINA YA WASIMAMIZI WA MAUDHUI, WASIMAMIZI WA TEHAMA NA MAKARANI WA SENSA WALIOFAULU USAILI WA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA YA SENSA NA KUITWA KWENYE MAFUNZO

    July 27, 2022
  • HALMASHAURI NAMTUMBO YAGAWA PIKIPIKI 38 KWA MAAFISA UGANI NA USHIRIKA

    June 24, 2022
  • MABADILIKO YA TA TAREHE YA KUFANYA USAILI

    June 22, 2022
  • DC NAMTUMBO ATANGAZA KIAMA WATAKAOPOTOSHA ZOEZI LA SENSA

    June 02, 2022
  • Ona zote

Video

HOTUBA YA WAZIRI WA TAMISEMI
Video

Kurasa za Haraka

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Halmashauri ya Songea
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Nyasa
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru

Tovuti Mashuhuri

  • TAMISEMI
  • Ikulu ya Tanzania
  • Tume ya Utumishi wa Umma
  • Baraza la Mitihani
  • Tume ya ajira Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

    Anuani: S.L.P 55 NAMTUMBO

    Simu ya Mezani: 0252675008

    Simu ya Mkononi: 0765142640

    Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

    • Maswali ya mara kwa mara
    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.