• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Complaints |
    • Gms |
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu ya Halmashauri
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji/Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Mipango, Uchumi na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Utumishi na Utawala
      • Maji
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • TASAF
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Fursa za Kilimo
    • Fursa za ufugaji
    • Fursa za Madini
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokalika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo za Halmashauri
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
    • Taarifa
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma/Vyombo Mbalimbali vya Habari
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali

DC NAMTUMBO ATANGAZA KIAMA WATAKAOPOTOSHA ZOEZI LA SENSA

Tarehe ya Kuweka: June 2nd, 2022


Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Dkt Julius Kenneth Ningu amewataka wananchi kuwabaini wanaopotosha zoezi la Sensa katika maeneo yao ili waweze kuchukuliwa hatua .

Akizungumza na wajumbe wa kamati ya sensa ngazi ya  wilaya Dkt Ningu aliwataka  wajumbe wa kamati kuhakikisha wanafuatilia kwa karibu wilayani humo kubaini wananchi wanaopotosha zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajia kufanyika mwezi agusti mwaka huu.

Dkt Ningu pamoja na kuwaagiza wajumbe wa kamati alidai ziara ya mikutano katika kata 21 za Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo kuhamasisha zoezi la Sensa litaanza  kwa Lengo la kutoa elimu kwa wananchi pamoja na kusikiliza changamoto toka kwa wananchi zinazoweza kuathiri zoezi la sensa lisifanyike kwa ufasaha na kuzipatia ufumbuzi wake

Aidha mkuu wa wilaya ya Namtumbo aliwaambia wajumbe kuwa zipo taarifa za wilaya katika sensa ya mwaka 2012 kuwa kulikuwa na watu kazi yao kubwa ilikuwa kupotosha wananchi kuhusu Sensa ya watu na makazi na kwa sensa ya mwaka huu mkuu wa wilaya huyo alisisitiza kutowaruhusu watu kupotosha wananchi juu ya zoezi la sensa na watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria dhidi yao.

Katibu wa mbunge Zuberi Lihuwi aliyemwakilisha Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Vitta  Rashid Kawawa katika kikao hicho alimthibitishia mkuu wa wilaya kuwa katika sensa ya mwaka 2012 changamoto ya kuwepo kwa vikundi vya watu kuhamasisha wananchi kutokuhesabiwa lilikuwa kubwa na kuathiri upatikanaji sahihi wa takwimu za watu wa wilaya ya Namtumbo.

Lihuwi alidai yeye haamini  takwimu ya idadi  ya watu iliyopatikana katika sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 ilikuwa na uhalisia katika wilaya ya Namtumbo kwani idadi kubwa ya wananchi hawakuhesabiwa kutokana na kikundi hicho kupotosha wananchi kuhusu zoezi la sensa.

Glory Lwomile Hakimu mfawidhi wa wilaya ya Namtumbo naye pia alimthibitishia mkuu wa wilaya kuwa kikundi cha watu kinachohamasisha wananchi wa Namtumbo kutohesabiwa kinatoka nje ya wilaya ya Namtumbo akitolea mfano wa sensa ya mwaka 2012 kuwa yeye alikuwa katika wakati mgumu baada ya mahakama kuwaweka mahabusu   baadhi ya wananchi ambao sio wakadhi wa Namtumbo baada ya kubainika kuhusika na kuwahamasisha wananchi kutoshiriki zoezi la sensa alisema Hakimu huyo.

Mratibu wa Sensa  wilaya ya Namtumbo Kuno Ntini aliwaambia wajumbe kuwa maandalizi ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 katika wilaya ya Namtumbo yanaenda vizuri ambapo mpaka sasa kazi zilizofanyika ni pamoja na uundaji wa kamati za sensa ngazi za wilaya,kata ,vijiji na vitongoji umekamilika,ubandikaji wa matangazo ya ajira ya muda ya sensa ya mwaka 2022 katika kata zote zoezi ambalo nalo lilienda vizuri na utoaji wa ufafanuzi juu ya changamoto za waombaji wa nafasi za ajira za muda ya sensa nalo lilienda vizuri.

Ntini alidai waombaji wa ajira ya Muda ya sensa katika mfumo wa maombi kadiri ya  tume ya taifa ya  takwimu  (NBS)wilaya ya Namtumbo waombaji wamefikia 2,277 ikiwa walioomba ukarani 1,741,usimamizi wa mahudhui 481 na usimamizi wa Tehama 55 huku maombi yaliyotumwa NBS ni 2047 na maombi 230 yanasubiria ukamilishaji wa fomu namba 1 alisema Ntini.

Sensa ya mwaka huu 2022 katika wilaya ya Namtumbo mkuu wa wilaya  amedai hataruhusu kikundi cha watu kupotosha zoezi la sensa na watakaobainika kufanya hivyo watakamatwa na kufikishwa mahakamani kwa zoezi la kuhujumu zoezi la sensa .

MWISHO

NA YEREMIAS NGERANGERA

NAMTUMBO

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WAOMBAJI WA KAZI YA MUDA YA SENSA WALIOFAULU USAILI NA KUITWA KWENYE MAFUNZO July 27, 2022
  • TAARIFA KWA UMMA June 27, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WAOMBAJI WA KAZI YA MUDA YA SENSA WALIOFAULU USAILI NA KUITWA KWENYE MAFUNZO July 27, 2022
  • MABADILIKO YA TAREHE YA KUFANYA USAILI June 22, 2022
  • Ona zote

Habari Mpya

  • ORODHA YA MAJINA YA WASIMAMIZI WA MAUDHUI, WASIMAMIZI WA TEHAMA NA MAKARANI WA SENSA WALIOFAULU USAILI WA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA YA SENSA NA KUITWA KWENYE MAFUNZO

    July 27, 2022
  • HALMASHAURI NAMTUMBO YAGAWA PIKIPIKI 38 KWA MAAFISA UGANI NA USHIRIKA

    June 24, 2022
  • MABADILIKO YA TA TAREHE YA KUFANYA USAILI

    June 22, 2022
  • DC NAMTUMBO ATANGAZA KIAMA WATAKAOPOTOSHA ZOEZI LA SENSA

    June 02, 2022
  • Ona zote

Video

HOTUBA YA WAZIRI WA TAMISEMI
Video

Kurasa za Haraka

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Halmashauri ya Songea
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Nyasa
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru

Tovuti Mashuhuri

  • TAMISEMI
  • Ikulu ya Tanzania
  • Tume ya Utumishi wa Umma
  • Baraza la Mitihani
  • Tume ya ajira Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

    Anuani: S.L.P 55 NAMTUMBO

    Simu ya Mezani: 0252675008

    Simu ya Mkononi: 0765142640

    Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

    • Maswali ya mara kwa mara
    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.