DC NAMTUMBO ATOA MAAGIZO MAZITO KWA MAFUNDI
Mafundi wanaotekeleza ujenzi wa miradi wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma wametakiwa kufanyakazi Kwa kuzingatia muda na ubora wa majengo yanayojengwa.
Akizungumza na mafundi katika ziara ya kukagua ujenzi wa madarasa shule ya msingi Mchomoro ,shule ya msingi masuguru ,ujenzi wa shule ya Sekondari Dkt.Samia Suluhu Hassan, Shule ya Sekondari Pamoja na ujenzi wa madarasa matano na mabweni ya shule ya watoto wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Namtumbo Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Ngollo Malenya amewataka mafundi kuacha Kutoa visingizio .
Malenya amemwagiza mhandisi wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo kushirikiana na ofisi yake Ili kuwachukulia hatua mafundi wote wanaochelewesha ujenzi katika wilaya ya Namtumbo.
Aidha Malenya alibaini mafundi kuchelewesha kazi kunakofanywa na mafundi wakuu kuwa na mafundi wachache maeneo ya kazi licha ya kuwepo Kwa vifaa katika maeneo mengi
Robert Magesa mhandisi wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo alimwambia mkuu wa wilaya kuwa uchache wa mafundi ndio sababu ya kuchelewesha mradi kwani katika maeneo mengi vifaa vipo lakini mafundi wachache hukwamisha uharakishwaji wa mradi.
Ziara ya Mkuu wa wilaya ya Namtumbo ilifanyika Ili kufuatilia maagizo aliyotoa Kwa mafundi katika ziara yake ya hivi karibuni aliyotaka kufanyika baadhi ya marekebisho ambayo mafundi hao walitakiwa kuyafanyia kazi lakini mafundi wameonesha kuchelewesha kutekeleza maagizo na kuamua kuanza kuwachukulia hatua mafundi hao.
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.