• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Complaints |
    • Gms |
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu ya Halmashauri
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji/Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Mipango, Uchumi na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Utumishi na Utawala
      • Maji
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • TASAF
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Fursa za Kilimo
    • Fursa za ufugaji
    • Fursa za Madini
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokalika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo za Halmashauri
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
    • Taarifa
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma/Vyombo Mbalimbali vya Habari
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali

DC NAMTUMBO AWASIMAMISHA KAZI WENYEVITI WATANO WA VITONGOJI

Tarehe ya Kuweka: May 4th, 2023

                     DC NAMTUMBO  AWASIMAMISHA KAZI WENYEVITI  5  WA VITONGOJI.

Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Ngollo Ng’waniduhu Malenya  amewasimamisha kazi wenyeviti  wa tano wa vitongoji  wa mamlaka ya mji mdogo wa lusewa kwa tuhuma ya kuhujumu zoezi la kuwaondoa  wafugaji  katika mamlaka ya mji mdogo wa Lusewa.

Malenya  alifikia uamuzi huo baada ya kusikiliza kero za wananchi wa mamlaka ya mji mdogo wa Lusewa waliodai  zoezi la kuwaondoa wafugaji katika maeneo  ya mamlaka  hiyo linakwamishwa  na viongozi wa mamlaka  .

Rajabu  Sangana  katibu wa chama cha Demokrasia na maendeleo wilaya ya Namtumbo pamoja na kumpongeza mkuu wa wilaya ya Namtumbo kwa kuanzisha kampeni ya kuwaondoa  wafugaji wilayani ya Namtumbo, katika mamlaka ya mji mdogo wa Lusewa  zoezi hilo linakwamishwa na viongozi wa mamlaka kwa kuwasiliana na wafugaji katika kila mpango unaopangwa na viongozi ngazi ya wilaya.

Sangana  alimhakikishia mkuu wa wilaya huyo kuwa kila mipango inayofanyika ya kutaka kuwakamata wafugaji hao ,wafugaji hao wanakuwa wanataarifa  na mipango yote inayofanyika viongozi hao huwasiliana nao na wafugaji hao hutoweka katika maeneo hayo na baadae hurudi katika maeneo hayo kupitia mawasiliano yanayofanyika na viongozi hao.

Kasmi Thabiti  Halidi naye mkazi wa mamlaka ya mji mdogo wa Lusewa alimthibitishia mkuu wa wilaya huyo kuwa viongozi hao wa mamlaka  sio waaminifu kutokana na kutosimamia  maamuzi ya vikao na badala yake huwasiliana na wafugaji  hatua kwa hatua na kuwathibitishia kuwa hawawezi kuondoka katika maeneo hayo ya Mamlaka na kuathiri maeneo ya kilimo  ya wananchi.

Mkuu wa wilaya huyo baada ya kupokea kero za tuhuma hizo kutoka kwa wananchi wao, aliwataka viongozi  hao mmoja mmoja kutoa maelezo yao kujibu tuhuma hizo zinazowakabili  kutoka kwa wananchi wao.

Alphani Kanduru  Ngurukuru  mwenyekiti wa  kitongoji cha Zanziba na Shazari Abeid  Chikwemba mwenyekiti wa kitongoji cha Ushirika wote kwa pamoja  walimwambia mkuu wa wilaya huyo kuwa hawapo tayari kueleza tuhuma zilizoelekezwa kwao ,walimwomba mkuu wa wilaya kufanya uchunguzi ili wakibainika kuwa wenyeviti hao kuhusika  na tuhuma hizo sheria ichukua mkondo wake

‘’Nawasimamisha kazi  kupisha uchunguzi “alisema mkuu wa wilaya ya Namtumbo huku akiwataka  viongozi  hao kutoa ushirikiano kwa kamati ya uchunguzi atakayoiunda ili iweze kufanyakazi yake bila kumwonea mtu yoyote.

Wenyeviti wa vitongoji  waliosimamishwa kazi ni mwenyekiti wa kitongoji cha Lusewa  Juma Sandali,Muhamudu Matumbi mwenyekiti wa kitongoji cha Kwizombe,Adamu Kalela  mwenyekiti wa kitongoji cha Mchajila ,Shadhari Chikwemba mwenyekiti wa kitongoji cha Ushirika  na Alphan Ngurukuru Mwenyekiti wa kitongoji cha Zanziba.

Mkuu wa wilaya ya Namtumbo alianzisha zoezi la kuwaondoa wafugaji katika maeneo yasiyorasmi  kwa kuunda kamati iliyowahusisha wananchi wa kijiji hicho ili kuwaondoa  wafugaji hao lakini kamati hiyo kwa mujibu wa wananchi hao hawakufanya kazi yao ipasavyo kwa kuwa ilikuwa inahujumiwa  katika mipango yake na viongozi hao kwa kuwasiliana na wafugaji katika kila hatua na kuwathibitishia kuwa watawasimamia kuhakikisha kuwa hawaondoki katika maeneo  hayo.

Mwisho..

 

Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA KWA WATENDAJI WA VIJIJI NA MADEREVA April 13, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA KWA WATENDAJI WA VIJIJI NA MADEREVA April 13, 2023
  • ORODHA YA MAJINA YA WAOMBAJI WA KAZI YA MUDA YA SENSA WALIOFAULU USAILI NA KUITWA KWENYE MAFUNZO July 27, 2022
  • TANGAZO LA AJIRA KWA WATENDAJI WA VIJIJI NA MADEREVA April 13, 2023
  • Ona zote

Habari Mpya

  • MNADA WA UFUTA WAIBUA SHANGWE NA NDEREMO KWA WAKULIMA NAMTUMBO

    May 25, 2023
  • DC NAMTUMBO AWAAMURU WAFUGAJI KUONDOKA KWA MASLAHI MAPANA YA TAIFA

    May 08, 2023
  • DC NAMTUMBO AWAONYA WAFUGAJI

    May 05, 2023
  • DC NAMTUMBO AWASIMAMISHA KAZI WENYEVITI WATANO WA VITONGOJI

    May 04, 2023
  • Ona zote

Video

HOTUBA YA WAZIRI WA TAMISEMI
Video

Kurasa za Haraka

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Halmashauri ya Songea
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Nyasa
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru

Tovuti Mashuhuri

  • TAMISEMI
  • Ikulu ya Tanzania
  • Tume ya Utumishi wa Umma
  • Baraza la Mitihani
  • Tume ya ajira Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

    Anuani: S.L.P 55 NAMTUMBO

    Simu ya Mezani: 0252675008

    Simu ya Mkononi: 0765142640

    Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

    • Maswali ya mara kwa mara
    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.