DC NAMTUMBO AWATAKA MAFUNDI KUZINGATIA MICHORO
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Ngollo Malenya amewataka mafundi wanaojenga miradi ya ujenzi katika wilaya ya Namtumbo kuzingatia michoro waliyopewa Ili kutekeleza ujenzi wa miradi hiyo na kuondoa maswali au sintofahamu zinazoweza kujitokeza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo.
Akiongea na mafundi ,kamati za ujenzi na viongozi wa Serikali katika ujenzi wa shule ya msingi mchomoro,shule mpya ya msingi masuguru pamoja na Shule ya Sekondari ya Dkt Samia Suluhu Hassan ,Malenya aliwasizitizia mafundi na viongozi wanaosimamia miradi hiyo kusimamia vipimo vilivyoko katika michoro na sio vinginevyo.
Malenya amefanya ziara ya kutembelea miradi ya ujenzi katika shule ya msingi Mchomoro, Masuguru pamoja na Sekondari ya Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kujionea changamoto na Kisha kuzipatia ufumbuzi
Ili kazi hizo za ujenzi ziweze kutekelezwa Kwa ufanisi mkubwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.