KAMATI YA SIASA YAPONGEZA USIMAMIZI WA MIRADI NAMTUMBO
Kamati ya siasa Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma Oddo Kirian Mwisho wamepomgeza usimamizi wa miradi wilayani Namtumbo.
Akiongea wakati wa ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa madarasa shule ya msingi Mchomoro, Shule ya msingi masuguru ,shule ya Sekondari Pamoja na Shule ya msingi Suluti kukagua ujenzi wa miundombinu ya madarasa alisema anapongeza usimamizi mzuri wa miradi hiyo .
Komred Oddo Mwisho alidai uwepo wa usimamizi wa miradi mzuri unaoendana na matumizi sahihi ya fedha zinazoletwa na Serikali itasababisha wananchi kuiamini Serikali Yao inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi chini mwenyekiti wake Raisi Dkt Samia Suluhu Hassan.
Aidha mwenyekiti huyo alifafanua kuwa uwepo wa utekelezaji wa miradi
yenye fedha nyingi bila kuchangisha wananchi kama huko nyuma inakifanya Chama Cha Mapinduzi kushinda uchaguzi mkuu wa Serikali za mitaa mwakani pamoja na u chaguzi mkuu wa Raisi na wabunge mwaka 2025.
Pamoja na hayo aliwasizitizia viongozi wa wilaya ya Namtumbo kuhakikisha miradi inakamilika Kwa wakati Ili kuendana na malengo yaliyowekwa na Serikali ya kuyataka majengo hayo yaanze kutumika na wanafunzi .
Mkuu wa shule ya Sekondari ya Pamoja Amos Mapunda alimshukuru mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma Komred Oddo Mwisho Kwa kutembelea shule hiyo na kudai kuwa shule hiyo Kwa muda mrefu ilisahaulika lakini Kwa Sasa wamepewa fedha za kutosha kujenga madarasa ,vyoo na mabweni ya kutosha.
Hata hivyo Mapunda alimshukuru Raisi wa Jamhuri wa Muungano Kwa kuipa fedha nyingi shule hiyo kujenga madarasa ,vyoo pamoja na mabweni ambayo imeifanya shule hiyo kubadili sura yake kuwa na tofauti na majengo ya awali.
Mapunda pamoja na kuishikuru Serikali alimwambia mwenyekiti wa Chama Mkoa kuwa shule hiyo Kwa sasa itapungukiwa na bwalo la shule ,jengo la komputa pamoja na jengo la utawala .
Ziara ya Kamati ya siasa Mkoa wa Ruvuma ilikuwa ya siku moja ambapo walitembelea mradi wa ujenzi shule ya msingi Mchomoro,shule ya msingi masuguru,shule ya Sekondari Pamoja ,shule ya msingi Litola,shule ya msingi Mtelamwahi, shule ya msingi Suruti,pamoja na kituo Cha afya Ligera ambapo katika ukaguzi huo kamati imepongeza usimamizi wa miradi hiyo .
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.