KERO YA UPATIKANAJI MAJI YAPUNGUA NAMTUMBO
Utekelezaji wa miradi 15 ya maji katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma imepunguza Kwa kiasi kikubwa malalamiko ya upatikanaji wa maji yaliyokuwepo huko nyuma.
Kaimu meneja wa RUWASA katika wilaya ya Namtumbo Salumu Nachundu alisema kero za upatikanaji wa maji zimepungua baada ya kutekeleza miradi mingi ya maji na kuwawezesha kupata mahitaji ya maji katika maeneo Yao.
Nachundu alibainisha utekelezaji wa miradi 15 ya maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo iliyochangia kupunguza kero za upatikanaji wa maji Kwa wananchi.
Katika utekelezaji wa miradi hiyo Nachundu alisema ipo miradi imekamilika , ipo miradi imefika asilimia 65 na miradi mingine ipo katika hatua za awali za kuanza.
Hassan Ndomondo mkazi wa Kijiji Cha Mgombasi kata ya Mgombasi alisema kero ya upatikanaji wa maji katika Kijiji hicho zimepungua kutokana na serikali kutoa kiasi Cha shilingi 150,000,000 ili kusambaza maji katika Kijiji hicho na vijiji vya jirani vya Mtumbatimaji na Nangero.
Ndomondo alidai Hali ya upatikanaji wa maji Kwa sasa ni mzuri
kwani hakuna malalamiko ya uhaba wa maji Kama iliyokuwa huko nyuma alisema Ndomondo
Hali ya upatikanaji wa maji katika wilaya ya Namtumbo ilikuwa asilimia 65 lakini kwa sasa hali ya upatikanaji maji ni asilimia 71 ambayo imesaidia kupunguza kero ya upatikanaji wa maji katika wilaya ya Namtumbo.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.