MIFUGO MINGINE 508 YAKAMATWA NAMTUMBO
Ng”ombe 485,Kondoo 16, Mbuzi 4 na punda 3 wamekamatwa katika kijiji cha Kitanda wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wakiwa hawana vibali vya kuingiza mifugo hivyo mkoa wa Ruvuma wakitokea wilaya ya Malinyi mkoa wa Morogoro.
Mtendaji wa kijiji cha Kitanda Ayubu Muhuwa alisema mifugo hiyo imekamatwa katika eneo la hifadhi ya msitu wa kijiji cha kitanda “Mtaungana” uliotengwa na kijiji kwa ajili ya matumizi bora ya ardhi ya kijiji hicho cha kitanda.
Muhuwa alidai mifugo iliyokamatwa katika msitu huo ni Ng”ombe 485, kondoo 16,mbuzi 4 na punda 3 wakiwa katika eneo la msitu lililotengwa na kijiji kwa ajili ya matumizi bora ya ardhi na walipowahoji na mgambo wa kijiji hicho wafugaji hao walikiri kuwepo katika msitu huo bila vibali vyovyote na ndipo walipoamua kuwakamata na kuwafikisha katika kituo kidogo cha polisi katika kijiji cha Kitanda .
Efrem Mwale mwananchi wa kijiji cha kitanda alisema swala la wafugaji katika kijiji cha kitanda ni la muda mrefu kwani lilikuwa linafumbiwa macho na viongozi hali iliyowafanya wafugaji na mifugo yao kuingiza mifugo mara kwa mara kutoka Malinyi mkoa wa morogoro na kuingia mkoa wa Ruvuma kupitia kijiji cha Kitanda.
Mwale alisema anamshukuru mkuu wa mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas kwa kuanzia mpango wa kuzuia mifugo kuingia katika mkoa wa Ruvuma kwa kuwakamata wafugaji wanaoingiza mifugo mkoa wa Ruvuma bila vibali kutoka katika mamlaka husika hali ambayo inazaa matunda hisi sasa.
Aidha Mwale alidai viongozi wa vijiji walikuwa wanapigiwa kelele na wananchi kupitia mikutano ya hadhara wakilalamikia uingizaji wa wafugaji katika kijiji cha kitanda bila mafanikio kwa kile kilichoonekana kuwa baadhi ya viongozi walikuwa wananufaika na uwepo wa wafugaji hao katika maeneo ya vijiji alisema Mwale.
Afisa Mifugo wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Paul Ambokile pamoja na kukiri kukamatwa kwa wafugaji hao amewataka wafugaji kuzingatia taratibu ,kanuni na sheria za uingizaji au usafirishaji wa mifugo kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine kutafuta malisho.
Mifugo 508 inashikiliwa na jeshi la polisi kituo kidogo kilichopo katika kijiji cha kitanda huku utaratibu wa ulipaji wa faini ukisubiriwa na wafugaji hao kwa kosa la kuingiza mifugo katika mkoa wa Ruvuma kupitia kijiji cha kitanda wilaya ya Namtumbo na baada ya hapo utaratibu wa kurudisha mifugo hiyo ilikotoka utafanyika.
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: S.L.P 55 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0765142640
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.