• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Complaints |
    • Gms |
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu ya Halmashauri
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji/Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Mipango, Uchumi na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Utumishi na Utawala
      • Maji
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • TASAF
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Fursa za Kilimo
    • Fursa za ufugaji
    • Fursa za Madini
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokalika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo za Halmashauri
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
    • Taarifa
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma/Vyombo Mbalimbali vya Habari
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali

MKURUGENZI MAGESA ATOA SIKU 30 KUKAMILISHA MIRADI, WASIMAMIZI WATIA SAINI MKATABA WA MAKUBALIANO YA UTENDAJI KAZI (PERFORMANCE AGREEMENT CONTRACT).

Tarehe ya Kuweka: January 31st, 2026

MKURUGENZI MAGESA ATOA SIKU 30 KUKAMILISHA MIRADI, WASIMAMIZI WATIA SAINI MKATABA WA MAKUBALIANO YA UTENDAJI KAZI (PERFORMANCE AGREEMENT CONTRACT).


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, Ndg. Philemon Mwita Magesa, amefanya kikao kazi na Wasimamizi wa Miradi wa Halmashauri hiyo, ambapo wametia saini Mkataba wa Makubaliano ya Utendaji Kazi (Performance Agreement Contract) kwa lengo la kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilika kwa wakati, kwa ubora na kwa kuzingatia thamani ya fedha ya Serikali.


Kikao hicho kimewakutanisha Wakuu wa Idara na Vitengo vyote, Waganga Wafawidhi, Watendaji wa Kata, Wakuu wa Shule, Maafisa Elimu Kata pamoja na Walimu Wakuu kutoka kata zote 21 zilizopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo.


Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi Magesa ametoa siku 30 pekee kwa Wasimamizi wa Miradi kukamilisha miradi yote inayotekelezwa katika kata zao, akisisitiza kuwa hakutakuwa na uvumilivu kwa uzembe, uzorotaji wa kasi wala kukiuka viwango vilivyopangwa.


Aidha, Magesa amewataka Wasimamizi wa Miradi kuwabainisha wazi wazabuni na wakandarasi/fundi wote wanaosababisha usumbufu katika utekelezaji wa miradi, ikiwemo kuchelewesha usambazaji wa malighafi na kutotekeleza majukumu yao kwa mujibu wa mikataba, ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao bila kusita.

Mkataba huo wa Makubaliano ya Utendaji Kazi umetiwa saini tarehe 31 Januari, 2026, na umeanza rasmi kutekelezwa leo tarehe 1 Januari, 2026, ambapo baada ya muda uliopangwa kila msimamizi atawajibika kukabidhi mradi wake ukiwa umekamilika kwa asilimia 100.


Mkataba huo umetiwa saini na Wasimamizi wa Miradi na kushuhudiwa rasmi mbele ya Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, Wakili Walter Kaijage.


Hatua hiyo inalenga kuongeza uwajibikaji, ufanisi na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi wa Wilaya ya Namtumbo.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA NAMTUMBO January 09, 2026
  • Ona zote

Habari Mpya

  • MKURUGENZI MAGESA ATOA SIKU 30 KUKAMILISHA MIRADI, WASIMAMIZI WATIA SAINI MKATABA WA MAKUBALIANO YA UTENDAJI KAZI (PERFORMANCE AGREEMENT CONTRACT).

    January 31, 2026
  • MKURUGENZI MAGESA ATOA MAAGIZO MIRADI YOTE ITEKELEZWE KWA MFUMO WA USIKU NA MCHANA

    January 31, 2026
  • Mkurugenzi Magesa aongoza kikao cha Baraza la Robo ya Pili

    January 29, 2026
  • DC NGOLLO MALENYA AWAFARIJI WAHANGA WA RADI KATIKA KATA YA LUSEWA WILAYA YA NAMTUMBO

    February 21, 2025
  • Ona zote

Video

HOTUBA YA WAZIRI WA TAMISEMI
Video

Kurasa za Haraka

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Halmashauri ya Songea
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Nyasa
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru

Tovuti Mashuhuri

  • TAMISEMI
  • Ikulu ya Tanzania
  • Tume ya Utumishi wa Umma
  • Baraza la Mitihani
  • Tume ya ajira Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

    Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO

    Simu ya Mezani: 0252675008

    Simu ya Mkononi: 0767519181

    Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

    • Maswali ya mara kwa mara
    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.