NAMTUMBO WAPENDEKEZA VYANZO VIPYA VYA MAPATO
Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo limepokea Mapendekezo ya kuanzisha vyanzo vipya vya mapato kwa lengo la kuongeza mapato ya ndani.
Diwani wa kata ya Mkongo Daniel Nyambo alisema Mapendekezo hayo ya kuanzisha vyanzo vipya vya mapato ni mazuri lakini akaomba madiwani wapate muda wa kupitia vyanzo hivyo na baraza lijalo waweze Kutoa maamuzi.
Lukas Njogopa Diwani wa kata ya Rwinga naye Kwa upande wake alisema kuwa ni vyema waheshimiwa madiwani wakapitie vyanzo hivyo vya mapato Ili baraza lijalo waje na maamuzi mazuri
Katibu kamati ya mapato na afisa mipango na uratibu wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Musa Mumina katika taarifa yake kwenye baraza Hilo alifafanua vyanzo vipya vya mapato vinavyopendekezwa ni pamoja na ujenzi wa vibanda vya biashara,ujenzi wa karakana ya magari na mitambo,mashine ya kufuatilia tofali za saruji.,kiwanda Cha maji ya chupa na ujenzi wa shule ya Sekondari.
Hata hivyo aliongeza kuvitaja vyanzo vingine kuwa ni ununuzi wa mashine ya kuchakata kokoto,ujenzi wa ghala la kuhifadhia mazao,ujenzi wa stendi ndogondogo kwenye ngazi ya kata na vijiji pamoja na kituo Cha kuuza mafuta(Petrol station)
Amandus Chilumba afisa Serikali za mitaa kutoka ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Ruvuma aliwataka waheshimiwa madiwani Kushirikiana na wataalamu katika zoezi la ukusanyaji wa mapato.,mapato ndio uhai wa Halmashauri alisema Chilumba.
Chilumba pia alisisitiza kudumisha mahusiano ili kushughulikia mambo Kwa hekima, busara na akili katika kutatua changamoto zinazohitajika kutatuliwa .
Mapendekezo ya vyanzo vipya vya mapato katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo yatatolewa katika baraza la madiwani la robo yapili linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni kupisha madiwani hao kupitia Mapendekezo hayo na Kisha Kutoa maamuzi yenye tija Kwa Halmashauri hiyo.
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.