Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia generali Wilbert Ibuge alisema mkoa wa Ruvuma kwa kipindi cha mwaka mmoja wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan mkoa wa Ruvuma umefanikiwa kujenga madarasa 500 ya shule ya msingi na sekondari.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake brigedia generali Ibuge alisema mkoa wa Ruvuma kwa kipindi cha mwaka mmoja cha Rais Samia Suluhu Hassan mkoa umefanikiwa kujenga vyumba vya madarasa 500 ikiwa shule za sekondari madarasa 448 na shule za msingi shikizi 52.
Mkoa wa Ruvuma katika kipindi hicho uliongeza ujenzi wa mabweni 3katika shule maalumu za msingi kwa gharama za shilingi bilioni 10.24 kupitia mradi wa namba 5441 TCRP.
Shilingi 760,162,500 zimetumika kujenga ofisi 5 za wadhibiti ubora wa elimu Halmashauri za Tunduru,Songea manispaa,songea,Nyasa na Mbinga alisema mkuu wa mkoa huyo.
Hata hivyo brigedia generali Ibuge alitaja mapokezi ya fedha shilingi 13,148,789,2021.51 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Ruvuma.
Aidha katika kipindi hicho cha mwaka mmoja cha Mh. Rais Samia Suluhu Hassan mkoa wa Ruvuma umefanikiwa kutoa mikopo ya shilingi 3,038,893,921.00 kwa ajili ya kuwawezesha wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kiuchumi.
Pamoja na mafanikio hayo ya mwaka mmoja wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mkuu mkuu wa mkoa huyo amewataka wafanyabiashara na wajasiliamali walioko nje na ndani ya mkoa kutumia fursa za uwekezaji kutokana na mkoa huo kuwa na fursa nyingi za kiuchumi ambazo zinahitaji watu kuwekeza .
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.