SHULE 16 NAMTUMBO ZANUFAIKA NA WALIMU WA MAZOEZI YA KUFUNDISHA
Walimu wanachuo kutoka katika chuo cha ualimu Mtwara.kilichopo katika mkoa wa Mtwara wamesambazwa katika shule 16 za Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma kwa ajili ya kufanya mazoezi ya ufundishaji kwa vitendo.
Afisa elimu msingi wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Juma Fulluge alisema Halmashauri imepokea walimu wanachuo 59 kutoka katika chuo cha Ualimu Mtwara wamepokelewa na kupangiwa shule 16 za halmashauri ya wilaya ya Namtumbo.
Fulluge alitaja shule waliopata walimu wanachuo katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo kuwa ni shule ya msingi Masuguru,Songambele,Mchomoro,Litola,Selous,Rwinga,Njuga,Minazini pamoja na shule ya Msingi Ngwinde.
Alizitaja shule zingine kuwa ni shule ya msingi Migelegele,Lusenti,Mwenge,Namtumbo,Namwaya,Suluti na shule ya msingi libango ambazo zimepata walimu wanachuo kuanzia watatu mpaka wanne katika kila shule .
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Namwaya Alex Gadau amekiri kuwapokea walimu wanachuo 4 kutoka chuo cha ualimu Mtwara ambao wanafanya mazoezi ya kufundisha katika shule yake ya msingi Namwaya.
Gadau Aliwataja walimu wanachuo hao kuwa ni Masanja Mayala Rutalamila,Rashidi Bakari Mhina ,Oscar Sanke Mwamlenga na mwingine ni Samwel Musa Petro ambao wanafanya mazoezi ya kufundisha katika shule yake ya Namwaya.
Samwel Musa Petro na Oscar Sanke Mwamlenga walimu wanachuo wanaofundisha shule ya msingi Namwaya walisema wanafurahi kwa kupokelewa vizuri hasa kwa kupatiwa eneo nzuri kwa ajili ya maladhi , upatikanaji wa huduma ya chakula pamoja na ushirikiano wanaoupata kutoka kwa walimu waliopo shuleni hapo.
Mwisho
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.