• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Complaints |
    • Gms |
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu ya Halmashauri
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji/Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Mipango, Uchumi na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Utumishi na Utawala
      • Maji
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • TASAF
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Fursa za Kilimo
    • Fursa za ufugaji
    • Fursa za Madini
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokalika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo za Halmashauri
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
    • Taarifa
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma/Vyombo Mbalimbali vya Habari
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali

VIONGOZI WA JUMUIYA ZA WATUMIAJI MAJI WAPIGWA MSASA NAMTUMBO

Tarehe ya Kuweka: May 30th, 2022


Viongozi wa Jumuiya za watumiaji maji katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma zimepata mafunzo ya siku moja kuwawezesha kufanya kazi zao kwa kuzingatia sheria ,kanuni , taratibu  na miongozo iliyowekwa na serikali .

Akifungua mafunzo hayo mkuu wa wilaya ya Namtumbo Dkt Julius Kenneth Ningu aliwataka washiriki wa mafunzo kuzingatia mafunzo hayo na kisha kwenda kutumia maarifa watakayoyapata  katika kazi zao za kila siku .

Awali mratibu wa mafunzo kwa jumuiya za watumiaji maji RUWASA wilayani Namtumbo George Mswaya  alisema washiriki wa mafunzo hayo ni viongozi wa jumuiya za watumiaji maji kutoka katika vijiji ,kata vya wilaya ya Namtumbo.

Mswaya aliwataja   watendaji wa kata ,makatibu ,wahasibu na mafundi wa jumuiya za watumiaji maji katika wilaya hiyo kuwa ni washiriki wa mafunzo hayo  ili kuwajengea uwezo wa kiutawala katika kuimarisha jumuiya zao .

Viongozi wa jumuiya za watumiaji maji walifundishwa mada tano(5) ikiwemo ya utunzaji sahihi wa fedha iliyofundishwa na mhasibu wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Obed Mwasomola ,mada ya mazingira iliyofundishwa na afisa mazingira wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Kelvin Mnali ,mada ya sheria  ya huduma ya maji na usafi wa mazingira iliyofundishwa na mwanasheria wa Halmashauri hiyo Fabian Samweli  na  mada ya umuhimu wa kuchangia ankra za maji ikifundishwa na afisa maendeleo ya jamii wa Halmashauri hiyo Jesca Mwitinda.

Aidha mhandisi wa RUWASA wilaya ya Namtumbo David Mkondya aliwasisitizia washiriki wa mafunzo kwenda kuongeza watumiaji maji katika jumuiya zao, kwenda kuhakikisha jumuiya zao zinasajiriwa kisheria,kwenda kuhakikisha jumuiya zao zinakuwa na viongozi wanawake  na kuhakikisha  katika huduma za maji kunakuwa na mfumo wa kutibu maji kwa lengo la kutimiza vigezo vilivyowekwa na wafadhili wanaoshindanisha watumiaji maji, na jumuiya ya watumiaji maji inayokidhi vigezo  hulipwa 56,250kwa  kila mtumiaji maji katika jumuiya iliyokidhi vigezo hivyo.

Yasini Salumu Kayonga fundi na katibu wa bodi ya maji katika jumuiya ya kijiji cha matepwende Pamoja na kuipongeza RUWASA kwa kuwapa mafunzo hayo alidai mafunzo hayo yameongeza ari  ya kufanya kazi kwa kuzingatia sheria,kanuni ,taratibu na miongozo iliyowekwa na kuwafanya washiriki kwenda kufanya kazi zao  kwa kujiamini alisema Kayonga.

Mafunzo kwa viongozi wa jumuiya za watumia maji  wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma yalifunguliwa na mkuu wa wilaya ya Namtumbo Dkt Julius Kenneth Ningu  katika ukumbi wa UNICEF  uliopo katika kijiji cha Mkongo gulioni.

NA  YEREMIAS NGERANGERA

NAMTUMBO

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WAOMBAJI WA KAZI YA MUDA YA SENSA WALIOFAULU USAILI NA KUITWA KWENYE MAFUNZO July 27, 2022
  • TAARIFA KWA UMMA June 27, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WAOMBAJI WA KAZI YA MUDA YA SENSA WALIOFAULU USAILI NA KUITWA KWENYE MAFUNZO July 27, 2022
  • MABADILIKO YA TAREHE YA KUFANYA USAILI June 22, 2022
  • Ona zote

Habari Mpya

  • ORODHA YA MAJINA YA WASIMAMIZI WA MAUDHUI, WASIMAMIZI WA TEHAMA NA MAKARANI WA SENSA WALIOFAULU USAILI WA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA YA SENSA NA KUITWA KWENYE MAFUNZO

    July 27, 2022
  • HALMASHAURI NAMTUMBO YAGAWA PIKIPIKI 38 KWA MAAFISA UGANI NA USHIRIKA

    June 24, 2022
  • MABADILIKO YA TA TAREHE YA KUFANYA USAILI

    June 22, 2022
  • DC NAMTUMBO ATANGAZA KIAMA WATAKAOPOTOSHA ZOEZI LA SENSA

    June 02, 2022
  • Ona zote

Video

HOTUBA YA WAZIRI WA TAMISEMI
Video

Kurasa za Haraka

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Halmashauri ya Songea
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Nyasa
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru

Tovuti Mashuhuri

  • TAMISEMI
  • Ikulu ya Tanzania
  • Tume ya Utumishi wa Umma
  • Baraza la Mitihani
  • Tume ya ajira Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

    Anuani: S.L.P 55 NAMTUMBO

    Simu ya Mezani: 0252675008

    Simu ya Mkononi: 0765142640

    Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

    • Maswali ya mara kwa mara
    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.