WAGOMBEA 13 WA SHIVIWATA NAMTUMBO WAFANYIWA USAILI
Shirikisho la vyama vya walemavu (SHIVIWATA) wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma limewafanyia usaili wagombea 13 katika nafasi mbalimbali za uongozi waliojitokeza kugombea nafasi katika shirikisho Hilo .
Akiongea mara baada ya kumalizikia Kwa zoezi la usaili huo msimamizi wa uchaguzi wa shirikisho Hilo Godfrey Mwaulesi ambaye alimwakilisha mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo alisema kuwa waliojitokeza kujaza fomu ni 13 .
Mwaulesi alidai waliojitokeza kujaza fomu za uongozi katika nafasi ya Mwenyekiti walikuwa 4 ikiwa wanaume 3 na mwanamke 1 na waliofanyiwa usaili walikuwa wanaume 2na mwanamke 1.
Pia Mwaulesi alifafanua katika nafasi ya Katibu waliojitokeza kujaza fomu walikuwa 5 ikiwa wanaume 3 na wanawake 2 na waliohudhuria usaili walikuwa 3 ikiwa wanaume 2 na mwanamke 1.
Katika nafasi ya Mwekahazina nafasi hiyo fomu ilijazwa na mtu 1 na katika nafasi ya wajumbe fomu zilijazwa na wajumbe 4 ambapo katika hao wajumbe waliofanyiwa usaili walikuwa 2 ikiwa mwanaume 1 na mwanamke 1.
Mgombea nafasi ya uenyekiti Bakari Salimu Mhamba alisema akipewa ridhaa ya wajumbe kumchagua kuwa kiongozi wao atawatumikia walemavu wenzake Kikamilifu.
Zabiuna Ngonyani Kwa upande wake alisema amegombea nafasi ya Katibu na kuwaomba wajumbe wakati wa uchaguzi ukifika wamchague Ili aweze kuwatumikia Kwa kuwa ana uzoefu mkubwa wa nafasi hiyo.
Shirikisho la vyama vya walemavu (SHIVIWATA) wilayani Namtumbo inatarajia kufanya uchaguzi tarehe 30 mwezi Agosti mwaka huu 2023 Ili kupata viongozi wapya wa shirikisho .
Uchaguzi wa vyama vya walemavu (SHIVIWATA) unafanyika Kila baada ya miaka mitano ambapo mara ya mwisho uchaguzi huo ilifanyika mwaka 2019.
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.