Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Viunga vya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Ndg. Philemon Mwita Magesa amewataka wananchi wilayani Namtumbo kujitokeza kwa wingi kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 2024.
Magesa amewakumbusha Wananchi kauli Mbiu ya Mwaka Huu ya Uchaguzi Mdogo wa Serikali za Mitaa ni "Serikali za Mitaa,Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi"
Wito huo ameutoa Agosti 27,2024 Baada ya Kutamatika kwa Baraza la Madiwani la Kujadili Taarifa za Fedha za Hesabu za Mwisho za Mwaka wa Fedha 2023- 2024 wilayani hapa.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.