• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Complaints |
    • Gms |
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu ya Halmashauri
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji/Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Mipango, Uchumi na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Utumishi na Utawala
      • Maji
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • TASAF
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Fursa za Kilimo
    • Fursa za ufugaji
    • Fursa za Madini
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokalika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo za Halmashauri
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
    • Taarifa
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma/Vyombo Mbalimbali vya Habari
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali

WANANCHI KUHAMA KIJIJI KUKOSA UMEME NA MAJI

Tarehe ya Kuweka: November 19th, 2021

                                  

Wananchi wa kijiji cha Mbimbi kitongoji cha Nambanje  kilichopo katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wamedhamiria kuhama kijiji kutokana na sababu ya kukosa huduma ya maji na umeme katika mtaa wao kwa muda mrefu.

Mwenyekiti wa kijiji cha Mbimbi Yustus Nyoni aliwaambia waandishi wa habari akiwa ofisini kwake kuwa kitongoji chake kimoja kinachoitwa Nambanje katika kijiji hicho wananchi wake wamedhamiria kuhama kijiji hicho kutokana na kukosa umeme na maji katika kitongoji chao kwa muda mrefu huku vitongoji vingine vikiwa na huduma hizo.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Nambanje Batlazali Ngonyani alidai wananchi wa kitongoji chake walikubaliana katika kikao cha kitongoji hicho kuwa wahame kijiji hicho na kwenda kijiji cha Namabengo ili waweze kupata huduma muhimu za maji na umeme kama wananchi wengine .

Ngonyani alisema malalamiko yao ya kudai umeme na maji ni ya muda mrefu lakini hakuna kinachoendelea kwa sasa na ndipo wananchi wa mtaa huo kwa pamoja na katika kikao chao cha kitongoji walikubaliana kuhama kijiji cha mbimbi na kwenda kijiji cha Nambabengo.

Salum Nachundu kaimu meneja Ruwasa pamoja na kukiri kuwa kitongoji hicho kukosa maji alidai miundombinu ya maji iliharibiwa na mkandarasi aliyekuwa anatengeneza barabara ya Namabengo –Mbimbi na kilichotakiwa kijiji kufuatilia fidia kwa mkandarasi aliyeharibu miundombinu hiyo na kuirudisha kama mwanzo ili wananchi wa kitongoji hicho kiweze kuendelea kupata maji.

Nachundu ambaye pia ni mlezi wa kata ya Litola na fundi mfuatiliaji wa kata hiyo alidai kitongoji hicho kinakosa maji kutokana na bomba linalopeleka maji katika kitongoji hicho kukatwa na mkandarasi aliyekuwa anatengeneza barabara ya Namabengo mpaka mbimbi .

Mtendaji wa kijiji cha Mbimbi Bernadeta Luambano pamoja na mambo mengine alithibitisha kuwa wananchi wa kitongoji cha Nambanje wanahitaji kuhamia kijiji cha Namabengo kutokana na kukosa maji na umeme katika kitongoji chao

Kwa mujibu wa meneja wa Tanesco wilaya ya Namtumbo Philipo Joseph Komu alidai kitongoji hicho hakijafanyiwa upembuzi yakinifu na akakiri kupokea malalamiko ya wananchi wa kitongoji cha Nambanje yaliyowasilishwa kwake na mtendaji wa kijiji cha Mbimbi.

Kitongoji cha Nambanje kimepitiwa na nguzo za umeme kutoka kijiji cha Namabengo lakini kitongoji hicho hakijapata umeme huku vitongoji vingine vya kijiji cha mbimbi vimepatiwa umeme na kuibua hasira baada ya kuona umeme umepita katika maeneo ya kitongoji chao lakini wakiishia kuutazama ukipita na kutumiwa na vitongoji vingine vya kijiji chao.

Kijiji cha Mbimbi kipo katika kata ya Litola kikiwa na vitongoji sita na kati ya vitongoji hivyo vitongoji vitano vimepatiwa huduma ya umeme na maji lakini kitongoji cha Nambanje pekee katika kijiji hicho kimekosa huduma ya maji na umeme na kufikiria kuhama kijiji hicho ili kwenda Namabengo kufuata huduma za maji na umeme.

Mwisho.  

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WAOMBAJI WA KAZI YA MUDA YA USAJILI WA ANUANI YA MAKAZI NA POSTIKODI WALIOFAULU USAILI NA KUITWA KWENYE MAFUNZO KUANZIA TAREHE 01 - 02/04/2022 March 30, 2022
  • MAJINA YA WAOMBAJI WALIOCHAGULIWA KUFANYA USAILI WA AJIRA ZA MUDA ZA KUSAJILI ANUANI ZA MAKAZI March 15, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI (LINARUDIWA) December 21, 2021
  • Ona zote

Habari Mpya

  • MABOMBA YA CHUMA KUMALIZA KERO YA MAJI KIJIJI CHA KUMBARA NA LITOLA

    May 18, 2022
  • DC AWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI WATATU NAMTUMBO

    April 27, 2022
  • MWENGE WA UHURU WAPITIA MIRADI 9 YENYE THAMANI YA MILIONI 550 NAMTUMBO

    April 15, 2022
  • KAMANDA WA POLISI MKOA WA RUVUMA AZUNGUMZIA MAUAJI

    April 13, 2022
  • Ona zote

Video

HOTUBA YA WAZIRI WA TAMISEMI
Video

Kurasa za Haraka

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Halmashauri ya Songea
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Nyasa
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru

Tovuti Mashuhuri

  • TAMISEMI
  • Ikulu ya Tanzania
  • Tume ya Utumishi wa Umma
  • Baraza la Mitihani
  • Tume ya ajira Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

    Anuani: S.L.P 55 NAMTUMBO

    Simu ya Mezani: 0252675008

    Simu ya Mkononi: 0765142640

    Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

    • Maswali ya mara kwa mara
    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.