• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Complaints |
    • Gms |
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu ya Halmashauri
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji/Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Mipango, Uchumi na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Utumishi na Utawala
      • Maji
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • TASAF
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Fursa za Kilimo
    • Fursa za ufugaji
    • Fursa za Madini
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokalika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo za Halmashauri
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
    • Taarifa
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma/Vyombo Mbalimbali vya Habari
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali

Wanawake Namtumbo walalamikia ukatili wa kijinsia

Tarehe ya Kuweka: March 7th, 2024

WANAWAKE NAMTUMBO WALALAMIKIA UKATILI WA KIJINSIA

Pamoja na Hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali kuhusu kukomesha ukatili wa kijinsia ,wanawake Wilayani Namtumbo wametumia Maadhimisho ya wiki ya kuelekea kilele Cha siku ya wanawake  Duniani kupaza sauti zao kulalamikia ukatili wa kijinsia.


Kwa Mujibu wa Risala ya wanawake wa Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma  Kwa mgeni Rasmi Ngollo Malenya ambaye  ni Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo wanawake hao wameendelea kulalamikia matendo ya ukatili wa kijinsia hasa Kwa wanawake waishio vijijini.


Risala iliyosomwa na Loema Thomas Safari ilitamka bayana kuwa wanawake Wilayani humo bado wanafanyiwa ukatili wa kijinsia ikiwemo kunyanyaswa, kukandamizwa, kufanyiwa vitendo viovu visivyostahili Kwa binadamu.


Aidha katika taarifa hiyo imeeleza kuwa wanawake wa vijijini Wilayani humo hunyimwa uhuru wa kutoa maamuzi kuhusu kupanga matumizi ya mapato yatokanayo na mazao waliyolima,kufanyishwa kazi Bila kupumzika ,kupigwa na hata kufukuzwa kwenye ndoa na pengine kunyang'anywa Mali.


Kwa Mujibu wa wanawake hao walisema kutokana na matendo hayo ya ukatili familia nyingi huwa duni kiuchumi ,familia kufarakana ,kupotea Kwa amani katika familia na kusababisha watoto wa mitaani na vijana kuzagaa mijini na mwishowe hujikita katika vitendo visivyokuwa vya kimaadili .


Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Peres  Kamugisha  pamoja na kuwapongeza wanawake wa Wilaya ya Namtumbo Kwa kuazimisha siku ya wanawake kiwilaya aliitaka Jamii kuwekeza katika watoto wa kike akiamini kuwekeza Kwa mtoto wa kike Kuna faida kubwa.


Kamugisha aliwaambia wanawake kuwa katika Nchi yetu wanawake  wamedhihirisha kuwa ni viongozi thabiti na mahiri kuanzia kwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mwanamke ,viongozi wengine wanawake waliopewa nyadhifa mbalimbali  wanaonesha kumudu vyema nafasi zao alisema Kamugisha.


Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Ngollo Malenya pamoja na kumshukuru Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan Kwa kuwawezesha wanawake kwa kuwapa mikopo kupitia mfuko wa maendeleo Kwa wanawake wenye thamani ya shilingi 287,680,000 toka mwaka 2015 mpaka mwaka 2024 alisema Serikali ya awamu ya Sita imedhamiria kuwaondolea Changamoto wanawake Kwa kufanikisha kujenga vituo viwili vya afya ,Ligera na Magazini ambavyo vimewaondolea wanawake Changamoto za upatikanaji wa huduma za afya hasa akina mama wajawazito.


Pamoja na hayo Malenya aliwaambia wanawake hao kuwa Nchi yetu imepiga hatua Mbele kwani imeshika namba 53 kati ya Nchi 144 zinazofanya vizuri katika masuala ya kijinsia kadiri ya taarifa jukwaa la uchumi Duniani kuhusu pengo la jinsia la mwaka 2016.


Malenya aliongeza Serikali imekamilisha ujenzi wa Sekondari ya Kisasa ya wasichana katika Wilaya yetu iliyogharimu shilingi 4,500,000,000 ili kuwawezesha watoto wa kike kupata elimu Bora.


Hata hivyo Malenya aliwataka wanawake wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi Kwa kuwa ni haki Yao kikatiba huku akiwahatarisha kujihadhari na ugonjwa wa ukimwi.


Awali Maadhimisho hayo yalianza Kwa Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo kugawia taulo za kike wanafunzi wa kike wa shule za msingi, sekondari Pamoja na chuo Cha ufundi stadi (VETA) zenye thamani ya shilingi milioni 2.


Kauli Mbiu ya Maadhimisho hayo Kwa mwaka huu ni  "Wekeza Kwa wanawake Kuharakisha maendeleo ya Taifa na ustawi wa Jamii.

Mwisho.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA NAMTUMBO January 18, 2025
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA NAMTUMBO MWAKA 2025 January 12, 2025
  • Ona zote

Habari Mpya

  • DC NGOLLO MALENYA AWAFARIJI WAHANGA WA RADI KATIKA KATA YA LUSEWA WILAYA YA NAMTUMBO

    February 21, 2025
  • WANANCHI NAMTUMBO WAMSHUKURU RAIS SAMIA

    January 06, 2025
  • MATREKTA aliyogawa Rais Samia yawanufaisha wananchi wa Wilaya ya Namtumbo, katika kuongeza Uzalishaji kwenye kilimo cha Kisiasa.

    January 06, 2025
  • Sukrani kwa Mhe.Rais wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan

    January 05, 2025
  • Ona zote

Video

HOTUBA YA WAZIRI WA TAMISEMI
Video

Kurasa za Haraka

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Halmashauri ya Songea
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Nyasa
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru

Tovuti Mashuhuri

  • TAMISEMI
  • Ikulu ya Tanzania
  • Tume ya Utumishi wa Umma
  • Baraza la Mitihani
  • Tume ya ajira Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

    Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO

    Simu ya Mezani: 0252675008

    Simu ya Mkononi: 0767519181

    Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

    • Maswali ya mara kwa mara
    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.