• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Complaints |
    • Gms |
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu ya Halmashauri
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji/Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi, Maliasili na Utalii
      • Mipango, Uchumi na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Utumishi na Utawala
      • Maji
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • TASAF
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Fursa za Kilimo
    • Fursa za ufugaji
    • Fursa za Madini
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokalika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo za Halmashauri
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
    • Taarifa
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma/Vyombo Mbalimbali vya Habari
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali

Baraza la wafanyakazi namtumbo lapitisha mapendekezo ya bajeti 2021/2022

Tarehe ya Kuweka: February 22nd, 2021


Baraza la wafanyakazi  katika  Halmashauri ya wilaya Namtumbo mkoani Ruvuma  limepitisha mapendekezo  ya  bajeti  ya Halmashauri  kwa mwaka wa fedha  2021/2022 ikikisiwa kukusanya  na kupokea jumla  ya Tsh .28,337,660,400 kutoka  vyanzo vya ndani,ruzuku kutoka serikali kuu na michango kutoka kwa wadau wa maendeleo.

Akisoma bajeti hiyo afisa  mipango wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo  bwana  Amos  Kanige  alisema  Halmashauri  inakisia kukusanya  kiasi cha Tsh 1,588,000,000 kutoka mapato ya ndani  na inakisia kupokea  Tsh 22,871,067,500 kutoka serikali kuu na Tsh.3,778,592,900 kama ruzuku  kutoka kwa wahisani.

Kanige  alifafanua  matumizi ya bajeti hiyo  kuwa  Tsh  18,043,444,000 itatumika  katika mishahara ,Tsh 2,858,693,000 kwa ajili  matumizi  mengineyo  na Tsh 7,337,660,400 kwa ajili  ya matumizi  ya miradi ya maendeleo.

Hata hivyo bwana  Kanige alisema katika mpango wa mapendekezo  ya bajeti  kwa mwaka 2021/2022 Halmashauri  imezingatia  sheria, kanuni,  taratibu na miongozo  iliyowekwa  na serikali katika kuandaa bajeti  hiyo na ushirikishwaji  wa wananchi  katika kutekeleza  miradi  mbalimbali ya maendeleo.

Kupitia bajeti  hiyo  Kanige alisema kutakuwa na  uboreshaji   wa huduma za elimu kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha sita, uboeshaji wa huduma za afya  kwa kuimarisha huduma za tiba na kinga ,kuimarisha vyanzo vya mapato ya ndani kwa kununua mashine 10 ya kukusanyia mapato,kuboresha stendi ya mabasi Namtumbo,kununua  na kusambaza  mbegu ya ufuta  na kuendeleza ujenzi wa soko la kisasa Namtumbo.

Aidha katika bajeti hiyo hiyo kutakuwa na uimarishaji wa huduma za kilimo na mifugo kwa kutoa huduma za ugani katika kata 21,ukarabati wa skimu za umwagiliaji na kujenga skimu 2 mpya ,ukarabati  wa machinjio moja,kufanya mpango wa matumizi bora ya ardhi , kuanzisha mnada wa mifugo pamoja na utoaji wa mikopo kwa vikundi 65 vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu  ikiambatana  na utoaji wa ruzuku  ya fedha  kwa kaya  4637 katika vijiji 42.

Katibu wa chama cha walimu wilayani  Namtumbo Mtamila Achikuo  pamoja na kupongeza mapendekezo ya bajeti  alidai amefurahishwa na kuingizwa katika bajeti  kikao cha baraza la wafanyakazi  tofauti  na bajeti  zilizopita ambazo zilisababisha malalamiko ya wajumbe wa kikao kutolipwa stahiki zao kwa wakati walipokuwa wakihudhuria vikao vya baraza la wafanyakazi  ambalo lipo kwa mujibu wa sheria.

Kwa mujibu wa Mwekahazina  wa Halmashauri ya wilaya Namtumbo  Pendo  Nyomeye  alisema mpaka kufika  juni 30,2020 mapato halisi yaliyokusanywa  ni Tsh 22,302,818,436.19 sawa na asilimia 91.79 ya fedha  iliyoidhinishwa  huku makusanyo ya mapato ya ndani yalikuwa 1,694,578,977.53 sawa na asilimia 119.6 ya lengo la mwaka ,mishahara  Tsh 16,434,760,623,23.matumizi mengineyo Tsh 1,313,064,100 na Tsh 2,860,414,735.40. kwa ajili ya maendeleo.

Matangazo

  • Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2021 kutoka katika shule mbalimbali za msingi za Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma December 18, 2020
  • Kimolo Secondary School Joining instruction December 18, 2020
  • Korido Secondary School Joining Instruction December 18, 2020
  • Lisimonji Secondary School Joining Instruction December 18, 2020
  • Ona zote

Habari Mpya

  • Naibu waziri aridhishwa ujenzi wa bweni ,bwalo namtumbo

    February 24, 2021
  • Baraza la wafanyakazi namtumbo lapitisha mapendekezo ya bajeti 2021/2022

    February 22, 2021
  • Familia 6 zapata pigo

    February 11, 2021
  • Mkurugenzi atoa maagizo mazito kwa watendaji

    February 10, 2021
  • Ona zote

Video

HOTUBA YA WAZIRI WA TAMISEMI
Video

Kurasa za Haraka

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Halmashauri ya Songea
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Nyasa
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru

Tovuti Mashuhuri

  • TAMISEMI
  • Ikulu ya Tanzania
  • Tume ya Utumishi wa Umma
  • Baraza la Mitihani
  • Tume ya ajira Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

    Anuani: S.L.P 55 NAMTUMBO

    Simu ya Mezani: 0252675008

    Simu ya Mkononi: 0765142640

    Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

    • Maswali ya mara kwa mara
    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki©2018Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.