Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Mheshimiwa Ngollo Malenya, amezitembelea familia mbalimbali zilizokumbwa na janga la kupigwa radi kwa watoto saba, ambapo watatu kati yao wamefariki dunia na wengine wanne wanaendelea kupatiwa matibabu katika Kituo cha Afya Lusewa, kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo.
Tukio hilo la kusikitisha limewaathiri zaidi familia moja, ambayo imepoteza watoto wawili kati ya hao saba waliopigwa radi na mtoto mmoja wa familia nyingine.
Mheshimiwa Malenya mewafariji majeruhi waliolazwa hospitalini na kushiriki katika kutoa mkono wa pole kwa familia za wafiwa kutoka vitongoji vya Mchangila, Ligunga, na Zanzibar.
Katika ziara yake, Malenya amewahimiza wazazi na wananchi kwa ujumla kuwa waangalifu hasa nyakati za mvua, akiwataka kujiepusha na kukaa karibu na miti ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na radi.
Mhe. Malenya pia amesisitiza mshikamano wa jamii katika kusaidiana na kuwafariji waliopatwa na msiba huu mzito, huku akiwataka wananchi kuwa na tahadhari zaidi dhidi ya majanga ya asili.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.