Wananchi wa kutoka Wilayani Namtumbo wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kugawa Matrekta matatu (3) ambayo yanawanufaisha wananchi wa tarafa tatu zilizopo katika Wilaya ya Namtumbo,
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mhe. Ngollo Malenya amewataka wakulima wa Wilaya ya Namtumbo kuendelea kuyatumia ipasavyo matrekta hayo katika kilimo ili kuongeza zaidi uzalishaji wa Mazao ya kimkakati ikiwemo mazao ya kibiashara ikiwemo Mbaazi, Ufuta, Soya na mazao mengine ya kibiashara.
Hata hivyo Ndg. Said Libaba mkulima wa kutoka kitongoji cha Suluti amefurahishwa na mpango wa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza thamani katika Sekta ya kilimo kwa kuwapatia wakulima vifaa vya kisasa Matrekta ambayo yanawanufaisha wananchi kulima wa Wilaya ya Namtumbo kuongeza uzalishaji wa Mazao mbalimbali.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.