BARAZA LA MADIWANI NAMTUMBO LAFANYA UCHAGUZI WA KAMATI ZA KUDUMU ZA HALMASHAURI.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Jumma Pandu alifungua kikao Kwa kusema kuwa kikao hicho Cha baraza la madiwani kina agenda moja kuu ya kufanya uchaguzi wa kamati za kudumu za Halmashauri.
Pandu alizitaja kamati zitakazofanya uchaguzi huo ni pamoja na kamati ya huduma ya uchumi ,ujenzi na Mazingira.,kamati ya elimu afya na maji , kamati ya fedha uongozi na mipango ,kamati ya ukimwi pamoja na kamati ya maadili.
Kabla ya uchaguzi huo kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Paul Ambokile alisoma barua kutoka ofisi ya Chama Cha mapinduzi ililiyokuwa ikiwasilisha jina la mgombea nafasi ya makamu mwenyekiti .
Aidha Kaimu Mkurugenzi alisoma Jina la Lukas Njogopa kuwa ni jina lililoteuliwa na Chama Cha Mapinduzi kugombea nafasi ya makamu mwenyekiti na kuwashauri wajumbe kupiga kura ya ndio au hapana Kwa kuwa mgombea nafasi hiyo ni mtu mmoja na kutoka kwenye Chama kimoja.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo aliwataka waheshimiwa madiwani kupiga kura ambapo kati ya madiwani 28 kura za ndiyo zilikuwa 28 na hapakuwa na kura yoyote ya hapana na kumfanya Lukas Njogopa kutangazwa kuwa ni makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Namtumbo Kwa kipindi Cha mwaka mmoja .
Baada ya zoezi hilo mwenyekiti alizitaka Kila kamati kufanya uchaguzi wa nafasi ya mwenyekiti wa kamati Ili kumpata mwenyekiti wa kamati aliyechaguliwa na wajumbe wa kamati husika.
Kaimu mkurugenzi Paul Ambokile alisoma matokeo ya uchaguzi kwa nafasi ya mwenyekiti kutoka Kila kamati ambapo alimtangaza Charles Chengula aliyepata kura 7 kuwa mwenyekiti wa kamati ya huduma ya uchumi ujenzi na mazingira Kwa kumshinda mpinzani wake Dani Nyambo aliyepata kura 6 kati ya kura 13 zilizopigwa.
Alimtangaza Said Zidadu kuwa mwenyekiti wa kamati ya Elimu afya na maji aliyepata kura 9 baada ya kuwashinda wapinzani wake Isdori Nyati aliyepata kuwa 3 na Kassimu Gunda aliyepata kura 1
Hata hivyo Ambokile alimtangaza Paul Fussi kuwa mwenyekiti wa kamati ya maadili Kwa kumshinda mpinzani wake Mrisho Mbawala aliyepata kura 1 kati ya kura 6 zilizopigwa na kumalizia na kamati ya ukimwi ambapo kamati hii Kwa Mujibu wa miongozo anayekuwa makamu mwenyekiti ndiye anakuwa mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ni Lukas Njogopa.
Zuberi Lihuwi mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi wilaya ya Namtumbo aliwaambia waheshimiwa madiwani kwenda kutekeleza majukumu Yao Kwa Ari na ustawi wa Halmashauri na Kwa kuzingatia mawazo ya watu waliowatuma.
Lihuwi Pia aliwataka madiwani hao kuisimamia Halmashauri ambayo alidai inachangamoto nyingi na hazina ulazima wa kuendelea kuwepo alisema Lihuwi.
Lakini pia Lihuwi aliwataka madiwani hao kwenda kufanya kazi katika maeneo Yao Kwa kuwa Chama kinategemea uwajibikaji wao katika nafasi zao na kuwaagiza madiwani hao kusimamia maamuzi Yao.
Amina Tindwa Afisa Serikali za mitaa kutoka katika ofisi ya Katibu tawala Mkoa wa Ruvuma aliwataka madiwani kwenda kuwa tumikia wananchi Kwa kusikiliza kero na kuzipatia majawabu Kwa kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo Yao.
kikao Cha baraza la madiwani kilifanyika Leo katika ukumbi wa Halmashauri ambapo kabla ya kumaliza kikao hicho mwenyekiti aliwatangaza wajumbe aliowateua watakaoungana na wenyeviti wa kamati kuwa wajumbe wa kamati ya fedha uongoxi na mipango kuwa ni Zamania Komba,Remna Nchimbi,Salimu Nyoni na Isdori Nyati kuungana na wenyeviti wa kamati kuwa wajumbe wa kamati ya fedha uongozi na mipango.
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.