CARBON YAMWAGA MAMILIONI YA HEWA UKAA NAMTUMBO
Kampuni ya Carbon inayohamasisha utunzaji wa Misitu Kwa ajili ya upatikanaji wa hewa ukaa imemwaga mamilioni Wilayani Namtumbo .
Priska Msuha Mkuu wa Kitengo Cha maliasili na uhifadhi wa Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo alisema Kampuni ya Carbon ilitoa jumla ya shilingi milioni 119 katika Wilaya ya Namtumbo Kwa ajili ya uhamasishaji utunzaji wa Misitu.
Msuha alidai fedha hizo zilitolewa Kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza zilitolewa milioni 18 Kila Kijiji kilipata milioni Moja huku jumuiya tatu za uhifadhi Wilayani humo Kila jumuiya ilipata milioni 3 ,huku Halmashauri hiyo ilipata kiasi Cha shilingi milioni 12,800,000.
Hata hivyo Msuha alifafanua malipo ya awamu ya pili kuwa Kampuni ya Carbon ilitoa milioni 54 ambapo katika vijiji 18 Kila Kijiji kilinufaika na kulipwa shilingi milioni 3 na jumuiya tatu za uhifadhi zilipata shilingi milioni 3 Kila jumuiya na Halmashauri ilipata milioni 10,200,000.
Afisa misitu wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Gravas Mwalyombo aliipongeza Kampuni ya Carbon Kwa kutoa fedha katika vijiji kuhamasisha utunzaji wa Misitu katika vijiji vyao ili kupatikana Kwa hewa ukaa.
Mwalyombo katika upande wa Kitengo Chake Cha misitu alidai kuwepo Kwa vijiji kuomba kuingizwa katika Mpango wa hewa ukaa baada ya kuona vijiji vilivyohifadhi misitu vinanufaika na mamilioni ya fedha kutokana na utunzaji wa Misitu.
Mwenyekiti wa Kijiji Cha Magazini Dandu Saidi Dandu Pamoja na kuishukuru Kampuni ya Carbon alikiri Kijiji chake kupokea fedha za hewa ukaa kutoka Kampuni ya Carbon Kwa ajili ya kufanyia Shughuli za maendeleo ya Kijiji hicho katika awamu mbili.
Dandu alibainisha matumizi ya fedha hizo katika Kijiji chake Cha Magazini ni Pamoja na kutengeneza madawati ya wanafunzi katika shule ya msingi Magazini ,kujenga choo Cha wanafunzi na kukarabati ofisi ya Kijiji Pamoja na Kununua vifaa vya ofisi ya Kijiji Cha Magazini kadiri ya maamuzi ya mkutano wa hadhara wa Kijiji hicho.
Kampuni ya Carbon imeahidi kuendelea kutoa fedha katika vijiji vya Wilaya ya Namtumbo Kwa ajili ya kuhamasisha utunzaji wa Misitu ili kuwezesha kupatikana Kwa hewa ukaa.
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.