Dc Namtumbo aagiza Ratiba utoaji elimu ya Lishe vijijini
Mkuu wa wilaya Ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Ngollo Malenya ameagiza kuwepo Kwa Ratiba Rasmi ya utoaji wa elimu ya Lishe Kwa wanawake wajawazito na jamii Kwa ujumla .
Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Lishe kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya sokoni katika mamlaka ya mji mdogo wa Namtumbo Perez Kamugisha afisa maendeleo ya jamii katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo alimwakilisha mkuu wa wilaya ya Namtumbo katika maadhimisho hayo na kusema kuwa Mkuu wa wilaya ameagiza kuwepo Kwa Ratiba za utoaji wa elimu za !ishe kwa wanawake wajawazito na Kwa. jamii
Kamugisha aliwataka wananchi wa wilaya ya Namtumbo kuzingatia Lishe kwani Kwa kufanya hivyo tutakuwa na jamii yenye afya Njema na yenye uwezo wa kufikiri katika kulileteea taifa maendeleo.
Aidha Kamugisha alitaja madhara ya kukosa Lishe Bora ni pamoja na jamii kuwa na ubwete, ukondefu pamoja na udumavu wa aki!I Kwa jamiii ambayo ni tegemeo Kwa ujenzi wa taifa.
Afisa Lishe wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Rehema Kivelia alitumia siku ya maadhimisho hayo Kutoa elimu ya Lishe Kwa jamii Kwa kuelezea makundi matano ya chakula Kwa kufafanua faida za makundi hayo katika Lishe na madhara ya kutotumia makundi hayo ya chakula katika Lishe
Hata hivyo Kivelia alisema timu ya wataalamu wa Lishe walipita mashuleni ,misikitini,makanisani kuhamasisha jamii kulima bustani za mbogamboga, matunda, ,ufugaji wa wanyama wadogo na Kisha Kutoa elimu ya Lishe Kwa jamii .
Afisa ustawi wa jamii katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Godfrey Mwaulesi pamoja na kuhimiza wananchi kuzingatia Lishe aliwaagiza maafisa ustawi katika vijiji na kata kusimamia vyema makuzi ya watoto katika maeneo Yao Kwa kuhakikisha watoto baada ya kuzaliwa wanasimamiwa vizuri Ili waweze kukua vizuri kiafya na kiakili.
Mwaulesi alifafanua kuwa watoto wengi wanaharibika mara baada ya kuzaliwa ,wazazi hawawazinagatii katika kuwapa Lishe Bora na malezi Bora Ili kuwawezeaha watoto hao kukua kimwili na kiakili na badala yake watoto huharibiwa Kwa kukosa malezi stahili alisema Mwaulesi.
Anna Hinju alimwakilisha Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Namtumbo alidai kuwa afya ndio msingi wa maendeleo katika jamii na aliitaka jamii kuzingatia Lishe Ili kuwa na afya Bora.
Hinju alisema Mkurugenzi Mtendaji amesaini mikataba mbalimbali na watendaji wa kata na vijiji Ili kusimamia utoaji wa afua za Lishe katika jamii.
Maadhimisho ya siku ya Lishe kitaifa yalifanyika katika viwanja vya sokoni mamlaka ya mji mdogo wa Namtumbo ambapo Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ilikuwa Lishe Bora Kwa vijana balehe chachu ya mafanikio Yao.
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.