DED NAMTUMBO ATEMBELEA MIRADI 18 YA UJENZI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Philemon Mwita Magesa alitembelea miradi 18 ya ujenzi yenye jumla ya shilingi 550,876,000.
Magesa alifafanua Lengo la kuitembelea miradi hiyo ni kukagua ujenzi ,kuzungumza na watumishi Pamoja na wananchi waliopo kwenye maeneo ya miradi inapotekelezwa ili kubaini Changamoto na mafanikio yaliyopo katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Hata hivyo Magesa alitaja vyanzo vya fedha zinazotekeleza miradi hiyo ni Seguip, Ruzuku toka serikali kuu, Mapato ya ndani ya Halmashauri, Swash Pamoja na mfuko wa Jimbo.
Katika ziara hiyo Magesa aliwataka wananchi ,watumishi waliopewa dhamana ya kusimamia miradi ya ujenzi kufanya hivyo ili majengo yanayojengwa yaendane na thamani halisi ya fedha inayotumika alisema Magesa
Kaimu Afisa Mipango na uratibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Gabriel Makuka alidai ukaguzi wa miradi hiyo ulifanyika katika kata Sita ikiwepo kata ya Hanga,Msindo,Namabengo,Litola,Rwinga na Mchomoro.
Hata hivyo Makuka alisema katika kata hizo vijiji 11 vilitembelewa Kwa kuzungumza na wananchi katika miradi kikiwemo Kijiji Cha Mtakanini,Msindo,Nambehe,Mlilayoyo,Ngwinde,Mdwema,Utwango ,Mbimbi,Nambalama Mchomoro na Mitaa miwili ya kata ya Rwinga alisema Makuka
Festo Kilowoko mkazi wa kata ya Namabengo alisema anafurahishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Philemon Magesa Kwa kutembelea na kukagua miradi ya ujenzi mara Kwa mara na kuzungumza na wananchi ,Watumishi katika maeneo iliyopo miradi ya ujenzi .
Ziara ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Philemon Magesa inaendelea katika kata na vijiji Wilayani humo kukagua miradi ya maendeleo kuzungumza na wananchi na watumishi ili kuhakikisha miradi inakamilika Kwa wakati na ujenzi unalingana na uthamani wa fedha iliyotolewa na Serikali.
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.