HALMASHAURI NAMTUMBO YAGAWIA PIKIPIKI 38 KWA MAAFISA UGANI NA USHIRIKA
Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma imewagawia pikipiki 38 aina ya boxer zilizotolewa na wizara ya kilimo katika Halmashauri hiyo hivi karibuni.
Kaimu afisa kilimo katika Halmashauri hiyo Michael Gambi alisema kuwa pikipiki hizo 38 zimegawiwa kwa maafisa ugani pamoja na maafisa ushirika wa wilaya hiyo.
Gambi alidai taratibu za kugawa pikipiki hizo kwa maafisa ugani na ushirika wa wilaya hiyo umefanywa na mkuu wa wilaya ya Namtumbo Dkt Julius Kenneth Ningu ndiye
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Chiriku Hamisi Chilumba pamoja na kuipongeza serikali kwa pikipiki hizo alisema pikipiki hizo zitarahisisha utendaji kazi wa maafisa ugani na ushirika katika maeneo yao ya kazi kwa kutoa huduma ya ugani kwa ufasaha.
Chilumba alidai zipo changamoto za maafisa ugani za kutowafikia wananchi kwa wakati kutokana na tatizo la usafiri, hivyo kitendo cha serikali kutoa pikipiki hizo zitaondoa changamoto hiyo ya muda mrefu kwa maafisa ugani .
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Dkt Julius Kenneth Ningu pamoja na kuipongeza serikali kwa kununua pikipiki hizo aliwataka maafisa kilimo na ushirika kwenda kuchapa kazi kwa kutoa huduma bora kwa wakulima ili kuonesha tofauti katika uzalishaji wa mazao ya kilimo.
Ningu aliwataka maafisa kilimo na ushirika kuhakikisha pikipiki hizo zinafanya kazi iliyokusudiwa na serikali katika maeneo yao ya kazi na sio vinginevyo.
Wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo hujishughulisha sana na kilimo hivyo kutolewa kwa pikipiki hizo itarahisisha wataalamu wa kil.imo na ushirika kutoa huduma ya utaalamu wa kilimo kwa wananchi wa wilaya ya Namtumbo na kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara katika wilaya hiyo.
NA YEREMIAS NGERANGERA
NAMTUMBO
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.