HII HAPA SIRI YA KUONGOZA USIMAMIZI WA MIRADI NAMTUMBO
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Generali Wilbert Ibuge aliipongeza Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo kwa kuongoza katika mkoa wa Ruvuma kwa usimamizi wa miradi ya ujenzi iliyofanywa katika wilaya hiyo.
Brigedia generali Ibuge aliyasema hayo katika kikao na wakuu wa idara wilayani Namtumbo mara baada ya ziara yake ya kukagua ujenzi wa madarasa shule za sekondari zilizopewa fedha za ujenzi za UVIKO 19 na kubaini kuwa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo kuongoza katika mkoa wa Ruvuma kwa kuwa na ujenzi uliokuwa wa viwango na ubora unaoridhisha ukilinganisha na Halmashauri zingine za Mkoa wa Ruvuma,.
Brigedia Generali Ibuge alidai katika ziara yake ya kukagua ujenzi wa madarasa yaliyopewa fedha za UVIKO19 Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo pekee katika mkoa wa Ruvuma ndiyo iliyofanikiwa kuweka Marumaru katika madarasa yake yote wilayani humo alisema aliyekuwa mkuu wa mkoa huyo.
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Dkt Julius Kenneth Ningu katika kikao hicho pamoja na kumshukuru aliyekuwa Mkuu wa mkoa kwa pongezi alisema ushirikiano wa usimamizi kati ya ofisi yake ,ofisi ya mkurugenzi na viongozi ngazi ya kata na vijiji ndio iliyosababisha mafanikio ya ujenzi huo kwa kiwango cha juu.
Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Namtumbo Chiriku Hamis Chilumba pamoja na kumshukuru aliyekuwa mkuu wa mkoa alitaja siri moja wapo ya kufanikisha ujenzi huo wa madarasa kuwa ni kugawa madarasa ya ujenzi kwa wakuu wa idara ambapo kila mkuu wa idara alipata shule ya kusimamia na kutakiwa kuwa katika eneo la ujenzi na kufuatilia ujenzi hatua kwa hatua na kutoa ripoti katika ofisi yake hali iliyosababisha ujenzi wa madarasa kuwa wa viwango na kuongoza katika mkoa wa Ruvuma
Chilumba pamoja na hayo alisema anawashukuru wakuu wa idara wote wa Halmashauri hiyo kwa kujituma na kushirikiana vyema na viongozi wa kata na vijiji katika kutekeleza miradi ya ujenzi kwa kiwango bora na kuifanya halmashauri yake kuongoza katika mkoa wa Ruvuma katika usimamiaji wa miradi.
Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo imepokea tena fedha za ujenzi wa madarasa shule za sekondari kiasi cha shilingi milioni 340 kutoka serikali kuu ili kujenga vyumba vya madarasa 17 katika shule zenye upungufu wa madarasa wilayani humo na kudai kuwa mbinu hizo za usimamizi wa ujenzi zitatumika ili kuhakikisha madarasa yanakuwa ya kiwango bora na kuongoza kimkoa tena.
NA YEREMIAS NGERANGERA
NAMTUMBO
.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: S.L.P 55 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0765142640
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.