KIJIJI CHA MDWEMA CHAPITISHA MPANGO WA MATUMIZI BORA YA ARDHI 2024/2034.
Wakiongea katika mkutano wa hadhara wa Kijiji hicho ,wananchi wa Kijiji Cha Mdwema walisema wanaridhia Mpango wa matumizi Bora ya ardhi ya Kijiji Chao.
Greyson Choma ni mwenyekiti wa Kijiji Cha Mdwema Pamoja na kuwashukuru wananchi wa Kijiji chake kuridhia kupitisha Mpango wa matumizi Bora ya ardhi ya Kijiji Chao , aliwashukuru zaidi wafadhili CARITAS waliogharimia Mpango huo .
Choma Pamoja na shukrani hizo aliwataka wananchi wa Kijiji hicho kufuata sheria,kanuni,miongozo na taratibu zilizowekwa katika kusimamia Mpango wa matumizi Bora ya ardhi .
Faustin Chuma mwananchi wa Kijiji Cha Mdwema Pamoja na kuridhia kupitisha Mpango huo aliiomba idara ya ardhi kupanda mawe kwenye mipaka kati ya Kijiji Chao na vijiji vingine ili kulinda ardhi Yao iliyotengwa Kwa ajili ya msitu ili wananchi wa vijiji vingine wasiingie katika maeneo hayo Kwa madai ya kutojua maeneo Yao.
Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Kelvin Mnali aliwaambia wananchi hao kuwa sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 inakataza kufanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji na maeneo ya milima huku akiwataka wananchi hao Kujua sheria hiyo katika kusimamia Mpango wa matumizi Bora ya ardhi ya Kijiji Chao.
Mary Albert Mratibu wa Mpango kutoka CARITAS ambao ndio waliofadhili Mpango huo alisema Kwa hatua za awali maeneo ya mipaka ya Kijiji hicho yatawekewa vibao kuonesha Shughuli inayotakiwa kufanywa katika eneo husika huku akiitaja idara ya ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kuandaa ramani na kupanda mawe kuonesha mpaka wa Kijiji hicho na vijiji vingine.
Zakaria Kapinga Afisa ardhi mteule wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo aliwaambia wananchi wa Kijiji Cha Mdwema kuwa Mpango wa matumizi Bora ya ardhi ya Kijiji chao utakuwa wa Miaka kumi kuanzia mwaka huu 2024 mpaka mwaka 2034 na baada ya Miaka 10 Mpango huo unaweza ukafanyiwa mapitio.
CARITAS ni Taasisi isiyo ya kiserikali ambayo inajishughulisha na vikundi vya ufugaji wa Nguruwe na kilimo Cha mazao kupitia vikundi vidogo vidogo vya wakulima wa Kijiji Cha Mdwema ambapo Taasisi hiyo inatumia kiasi Cha shilingi milioni 12 kukifanya Kijiji hicho kuwa katika Mpango wa matumizi Bora ya ardhi yake ya Kijiji.
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.