BARAZA LA MADIWANI NAMTUMBO LAPITISHA MAPENDEKEZO YA MPANGO NA BAJETI 2024/2025
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma limepitisha mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Kwa mwaka wa Fedha wa 2024/2025.
Afisa mipango ,uratibu na ufuatiliaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Musa Mumina alisema Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo inakisia kukusanya na kupokea jumla ya Tsh 35,475,103,000 ambapo kati ya hizo Tsh 10,810,840,000 ni fedha Kwa ajili ya miradi ya maendeleo,Tsh 20,505,300,000ni fedha Kwa ajili ya mishahara ,Tsh 1,325,123,000 ni fedha za ruzuku toka serikali kuu,Tsh 2,003,840,000ni fedha za mapato ya ndani yasiyolindwa na Tsh 830,000,000 ni mapato ya ndani lindwa.
Diwani wa kata ya Mkongo Daniel Nyambo alisisitiza bajeti iangalie uwezekano wa kuweka bajeti ya mafunzo Kwa waheshimiwa Madiwani ili wakajifunze Katika Halmashauri nyingine namna ya ukusanyaji wa mapato.
Nyambo alidai Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo inamaeneo mengi yanaendesha uchimbaji wa madini lakini hakuna diwani anayejua namna ya kukusanya mapato katika hayo machimbo na aliyoyaita machimbo bubu.
Diwani wa kata ya Ligera Sambode Mhongo alisema watendaji wa kata waliopewa dhamana ya kukusanya mapato wamezima data ,hatua za maksudi zinatakiwa kuchukuliwa ili kudhibiti watendaji ambao hawakusanyi mapato
na kuruhusu utoroshaji wa mapato katika maeneo Yao.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Namtumbo Acheni Maulidi Mwishehe Pamoja na mambo mengine aliwaambia waheshimiwa Madiwani kuwa kata ambayo haikusanyi mapato diwani wa kata hiyo Naye anahusika katika kudhorotesha ukusanyaji wa mapato Kwa kuwa yeye ndiye mwenyekiti wa maendeleo ya kata yake.
Aidha Mwishehe alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kubainisha kata zile ambazo hazikusanyi na katika Hilo Madiwani wanahusika katika kudhorotesha ukusanyaji huo alisema Mwishehe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Philemon Mwita Magesa aliwaambia waheshimiwa Madiwani kuwa swala la ukusanyaji wa mapato linahitajika nguvu ya pamoja kuanzia ngazi ya kitongoji,Kijiji,kata ,tarafa mpaka ngazi ya Wilaya.
Magesa alifafanua kuwa Bila Hela swala la kwenda mafunzo Kwa waheshimiwa Madiwani ni ndoto Kwa kuwa jibu ni rahisi hakuna fedha lakini pakiwa na fedha Yale yote yanayopangwa yanapangika alisema Magesa.
Pamoja na hayo Magesa aliwaomba waheshimiwa Madiwani kushirikiana katika swala la ukusanyaji wa mapato Kwa kuwa yeye anatembea na vipaumbele vitatu ikiwemo ya ukusanyaji mapato,usimamizi wa miradi Pamoja na utawala Bora.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Juma Pandu Naye aliwasisitizia Madiwani katika kata zao kusimamia Kwa karibu ukusanyaji wa mapato na kuahidi kumpa ushirikiano wa karibu kudhibiti utoroshaji wa mapato.
Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Kwa mwaka 2024/2025 umezingatia Dira ya Taifa ya maendeleo (2025) Sheria ya bajeti Na.11 ya mwaka 2015,mwongio wa uandaaji wa Mpango na bajeeti Kwa mwaka 2024/2025 uliotolewa na wizara ya fedha na mipango mwezi Novemba 2023
Mapendekezo hayo pia yamezingatia ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020/2025,na malengo ya maendeleo endelevu 2030mpango mkakati wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo 2021/2022-. 20205/2026 na mapendekezo ya vipaumbele kutoka ngazi ya kata,vijiji na maagizo mbalimbali ya viongozi.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.