MKUU WA WILAYA NAMTUMBO ATOA MAAGIZO MAZITO KWA VYOMBO VYA WATOA HUDUMA ZA MAJI.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Fransis Mgoloka alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo kwenye kikao Cha vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya Jamii na kutoa maagizo mazito .
Mgoloka aliagiza vyombo ambavyo havijaanza kuchangia huduma ya maji vianze mara Moja kuchangia, huku akiitaka taarifa ya uchangiaje huo ziwasilishwe ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Hata hivyo Mgoloka alimwagiza Meneja wakala wa maji na usafi wa Mazingira vijijini(RUWASA) Wilaya ya Namtumbo kusimamia Kwa dhati utekelezaji wa sheria namba 5 ya mwaka 2019 inayotaka kuunda Jumuiya ya watumia maji ili kuchangia huduma ya maji .
Pamoja na hayo aliagiza ofisi ya bonde za ziwa Nyasa na mto Ruvuma zihakikishe vyombo vya watumia maji vinakuwa na vibali vya kutumia maji huku akiwaagiza RUWASA kuendelea na zoezi la kuunda kamati zilizobaki katika vijiji.
Sheria namba 5 ya maji na usafi wa Mazingira ya mwaka2019 ilianzisha vyombo vya utoaji huduma ya maji ngazi ya Jamii Kwa Lengo la kusimamia miradi ya maji vijijini Kwa kuilinda,kuitunza na kuhamasisha uchangiaji huduma ya maji.
Kwa Mujibu wa taarifa ya RUWASA Kwa Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo ,ilidai Kwa mwaka 2023/2024 vyombo vya utoaji huduma ya maji ngazi ya Jamii vilifikia 18 lakini Pamoja na uundaji wa vyombo hivyo uchangiaji wa huduma hiyo inasuasua katika baadhi ya vyombo Licha ya kutolewa Kwa elimu kuhusu umuhimu wa kuchangia huduma ya maji ilisema taarifa hiyo.
George Mswaya Mratibu wa uundaji Vyombo vya utoaji huduma ya maji ngazi ya Jamii alisema RUWASA Inampango wa kuunganisha vyombo hivyo badala ya kuwa na vyombo vya utoaji huduma 18 vibaki 10 ili viweze kuwa na nguvu na uwezo wa kuwalipa wafanyakazi .
Dani Nyambo diwani wa kata ya Mkongo alishauri swala la kuunganisha vyombo vya utoaji huduma za maji sio suluhisho la wananchi kuchangia huduma hiyo Bali kuongeza nguvu za Pamoja ya kuwataka wananchi kuchangia huduma hiyo badala ya kuunganisha vyombo.
Nyambo alisema uwepo utaratibu wa wananchi kuchangia Kwa mkupuo wakati wa mavuno badala ya kidogokidogo kutokana na wananchi wa Namtumbo kutegemea mauzo ya mazao muda ambao wananchi wanakuwa na Hela ,hivyo ni vyema muda huo wachangie Kwa mkupuo alisema Nyambo.
Kikao Cha vyombo vya utoaji huduma ya maji ngazi ya Jamii kimefanyika katika ukumbi wa VETA Abasia ya Hanga ambapo Kwa taarifa ya RUWASA katika kikao hicho ilionesha uchangiaji wa huduma za maji sio wakuridhisha Hali iliyopelekea Kutoka Kwa maagizo mazito kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.