"MMEMTENDEA HAKI DKT. SAMIA SULUHU HASSAN" - VITA KAWAWA
Tarehe ya Kuweka: July 25th, 2024
Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Mhe. Vita Kawawa ameipongeza Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya namtumbo inayoongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ndg. Philemon Magesa Kwa Usimamizi mzuri wa Ujenzi wa Shule sekondari ya Wasichana ya Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyopo Wilayani Namtumbo katika Kata ya Rwinga.
Vilevile Mhe. Kawawa ameitaka Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kuendelea kufanya kazi kwa Ushirikiano ili waweze kutimiza Maendeleo makubwa na mikakati ya Kuhakikisha wanatekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi na Kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.