Mkuu wa mkoawa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameuagiza uongozi wa wilaya ya Namtumbo kuwauhakikishe inafanya tathimini ya kuwabaini wafugaji wote walioingia wilayanihumo bila kufuata taratibu, na ametoa siku 30 kuiondoa mara moja mifugo yao kwa walioingia pasipo kufuata taratibu na sivinginevyo.
Aidha mkuuwa mkoa kanali Laban Thomas amemwagiza kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma MarkoChilya, kuhakikisha kuwa wale wote waliohusika na tukio la mauwaji ya mkulimammoja na wafugaji 3 wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria harakaiwezekanavyo
Maagizo hayoyametolewa jana mchana na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas wakatiakiongea na mamia ya wananchi wakiwemo wakulima na wafugaji katika kata ya mkongogulioniiliopo wilaya ya Namtumbo ambao ulihudhuliwa na viongozi mbalimbali waserikali.
Alisema kuwakufuatia tukio lililo tokea novemba 7 mwaka huu la kuwepo mapigano kati yawakulima na wafugaji na kusababisha vifo vya watu 4 ni jambo ambalo linaletasura mbaya kwa serikali na wananchi wenyewe, hivyo ameutaka uongozi wa wilayaya Namtumbo uhakikishe unachukua hatua za haraka kwa kufanya tathimini yakuwabaini watu wa jamii ya wafugaji ambao walifika bila kufuata taratibuwaondoe mifugo yao haraka waipeleke wilaya ya Tunduru ambako kuna vitalukwaajili ya kufugia ng’ombe na mifugo mingine.
Mkuu wa mkoawa Ruvuma kanali Laban Thomas alifafanua zaidi kuwa jeshi la polisi mkoani humolihakikishe wanabaini wale wote ambao wamesababisha machofuko kwenye kata hiyo kwawanakamatwa ili kurudisha amani kwawananchi wa maeneo hayo ambapo kwa sasa wamegubikwa na hofu juu ya maisha yaokwa wakulima na wafugaji.
Kwa upandewake kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Marko Chilya akizungumza na Nipashejana alisema kuwa, Novemba 7 mwaka huu majira ya saa za mchana huko katika eneola kitongoji cha Ndilimila kata ya mkongogulioni, watu ambao ni jamii yawafugaji wa kabila la wamang’ati wakiwa na kundi la ng’ombe walifika kwenyebustani ya nyanya na mboga mboga ambako waliwaachia ng’ombe ambao walikula nakuharibu bustani yenye ukubwa wa zaidi ya hekali 1.
Alifafanuakuwa mmiliki wa bustani hiyo alipowaona wafugaji wakiwa na kundi la ng’ombealiwakataza lakini walikaidi na kuachia mifugo hiyo kwenye eneo la bustani yakebaadae waliondoka na mifugo yao kuelekea kwenye maeneo ya mashamba mengine.
KamandaChilya alifafanua kuwa, inadaiwa siku iliofuata mmiliki wa bustani hiyo aliefahamikakwa jina la Shaban Luambano(42) alikutwa akiwa ameuwawa kwa kuchomwa na mkukitumboni kisha kufunikwa na majani ya migomba ya ndizi .
Inadaiwa mkewake mdogo Sofia Husein wakati anakwenda kumwagilia maji kwenye bustani ndiealiegundua mwili wa mume wake ukiwa umefunikwa na majani ya migomba ya ndizi na baadae alitoa taarifa kwa uonozi waserikali ya kijiji, kisha polisi walifika kwenye eneo la tukio na sikuiliofuata watu 3 wa jamii ya wafugaji wa kabila la wamang’ati walikutwa wakiwawameuwawa na watu wasiojulikana ambapo aliwataja kuwa ni JacklineYegela(18),Kija Yegela(11) na Nkinga Ndila(13) pia ng’ombe zaidi ya 200wamekamatwa.
Na Yeremias Ngerangera
Namtumbo
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: S.L.P 55 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0765142640
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.