|
|
|
|
SONAMCU YAPATA MAFANIKIO UNUNUZI MAZAO STAKABADHI GHALANI.
Yeremias Ngerangera.....Namtumbo
Akiongea kwenye kikao Cha wadau wa mfumo wa stakabadhi ghalani meneja wa masoko wa chama kikuu Cha ushirika SONAMCU Zamakanaly Komba alisema chama hicho kimepata mafanikio makubwa katika kusimamia uuzaji wa mazao ya ufuta,mbaazi na soya katika misimu yote toka kuanzishwa Kwa mfumo wa stakabadhi ghalani Mkoani Ruvuma.
Komba alisema Moja ya mafanikio ni Ile Hali ya wakulima wenyewe kuuelewa mfumo wa stakabadhi ghalani na kunufaika na tija iliyopatikana kupitia kuuza mazao Yao Kwa mfumo huo
msimu wa 2022/2023 na 2023/2024.
Aidha Komba alifafanua faida nyingine ni Ile ya wanunuzi wa mazao hayo kulipa Kwa wakati na ndani ya siku zilizokubaliwa baada ya Kununua mzigo.
Hata hivyo Komba alitaja faida ya kuongezeka Kwa bei ya mazao ya ufuta, soya na mbaazi Kwa Kila msimu wa uuzaji wa mazao hayo huku vyama kulipa wakulima Kwa wakati Pamoja na Halmashauri kupata mapato yake Bila usumbufu wowote.
Pamoja na mafanikio hayo Komba alidai palikuwa na Changamoto ya wafanyabiashara kutorosha mazao Yao na kwenda kuuza nje ya mfumo wa stakabadhi ghalani ,aidha Changamoto ya mifuko kutokwenda Kwa wakati Kwa wakulima imepatiwa ufumbuzi wa Kudumu alisema Komba.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Juma Halfani Pandu alikiomba chama kikuu Kuharakisha mifuko Kwa wakulima ili kuondoa malalamiko ya kuchelewesha mifuko hiyo Kwa wakulima .
Pandu alidai hakuna shaka wakulima wa Wilaya ya Namtumbo wameukubali mfumo wa stakabadhi ya ghala na kujitokeza Kwa wingi kuuza mazao Yao kupitia mfumo huo.
Pia Pandu alikitaka chama kikuu kuendelea kutoa elimu Kwa wafanyabiashara ili waweze Kujua faida ya mfumo huo Kwa wakulima na sio maslahi Yao binafsi.
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.