KIKOKOTOO GUMZO MEI MOSI RUVUMA
Siku ya wafanyakazi Mkoani Ruvuma imeazimishwa katika Wilaya ya Tunduru ambapo vyama vya wafanyakazi vimepaza sauti zao kulalamikia Serikali kuhusu kikokotoo Kilichopo Kwa watumishi wa umma wakati wa kustaafu.
Akisoma Risala ya wafanyakazi Kwa Mgeni Rasmi katibu wa TUGE Mudathiri Ismail ambaye pia ni Mratibu wa Maadhimisho hayo alisema kikokotoo hakiwahusu waajiriwa wa zamani Kwa kuwa hakikuwa katika mikataba Yao ya ajira.
Ismail katika Risala hiyo alidai wafanyakazi wanafanya tathmini hatima ya ajira zao wakikinyoshea kidole kikokotoo ambacho kina watesa wafanyakazi hao .
Hata hivyo Ismail alifafanua kuwa mishahara ya wafanyakazi haikidhi mahitaji ukilinganisha na gharama halisi za maisha hivi Sasa .
Mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed ambapo Pamoja na mambo mengine alivishukuru vyama vya wafanyakazi Kwa kuandaa Maadhimisho hayo ya mei mosi na kujitokeza Kwa wingi kuhudhuria Maadhimisho hayo.
Kanali Abbas aliwataka waajiri katika Mkoa wa Ruvuma kujenga mazoea ya kutoka zawadi Kwa wiki,mwezi mmoja ,Sita Kwa wafanyakazi ili kuongeza morali ya kufanyakazi Kwa watumishi badala ya kusubiri siku ya wafanyakazi pekee.
Abbas aliwaambia wafanyakazi kuwa migogoro ya wafanyakazi inatokana na kutozingatia misingi ya utawala Bora ,kutokuwa na ushirikishwaji, usiri usio wa lazima na uamuzi usiozingatia haki Kwa watumishi alisema Kanali Abbas.
Hata hivyo aliwapongeza wafanyakazi kupitia Risala Yao kuthamini kazi kubwa ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt .Samia Suluhu Hassan katika ujenzi wa miradi mbalimbali Mkoani Ruvuma .
Pamoja na hayo yote Kanali Abbas amewaambia wafanyakazi kuwa Changamoto zote zilizotolewa zimepokelewa na ofisi yake na Changamoto zinazoweza kutatuliwa na ofisi yake zitafanyiwa hivyo na zile zingine zitapelekwa katika ngazi zingine zenye mamlaka.
Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mkoa wa Ruvuma yamefanyika katika Wilaya ya Tunduru ambapo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma alitoa zawadi ya fedha na vyeti Kwa wafanyakazi Bora wa Mkoa wa huo
Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi mwaka huu yamebeba kauli Mbiu isemayo "nyongeza ya mishahara ni msingi wa mafao Bora na kinga dhidi ya Hali ngumu ya maisha.
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.