TARURA NAMTUMBO YAIDHINISHIWA ZAIDI YA BILIONI 1.1
Wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma imeidhinishiwa kutumia shilingi 1,116,513,478.28 kutoka bodi ya mfumo wa barabara Kwa ajili ya matengenezo ya barabara na utawala.
Akitoa taarifa kwenye kikao Cha kamati ya ushauri wilaya (DCC) kwa niaba ya meneja wa TARURA Albert Mtimba alisema zaidi ya BILIONI 1.1 zimeidhinishwa kutumika katika mwaka wa fedha wa 2023/2024.
Mtimba alidai kiasi hicho Cha fedha kitatumika kuhudumia mtandao wa barabara wenye jumla ya kilomita 975.254 na madaraja 74.
Aidha Mtimba alifafanua kuwa katika kilomita 975.254 kilomita 4.603 ni barabara za Lami sawa na asilimia 0.47. na kilomita 280.369 barabara za changarawe sawa na asilimia 28.75.
Mtimba alisema kilomita 690.281 ni barabara za udongo ambapo ni sawa na asilimia 70.79za barabara za wilaya ya Namtumbo.
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo akiwemo diwani wa kata ya Litola Paulo Kamilius Fussi walihoji kitendo Cha utengenezaji wa barabara wakati wa masika na kusababisha usumbufu Kwa watumiaji wa barabara hizo.
Fussi alisisitiza umuhimu wa kuweka kifusi katika barabara zinazotengenezwa na kuziacha Bila kuweka kifusi kinasababisha barabara hizo kutopitika wakati wa mvua kutokana na utelezi alisema Fussi,
Mwenyekiti wa Baraza la ushauri la wilaya ya Namtumbo Ngollo Malenya Pamoja na mambo mengine aliwataka wakuu wa taasisi ,wakuu wa idara na vitengo kuzingatia maoni na ushauri uliotolewa na wajumbe wa Baraza katika taarifa zao, na kuwaagiza maoni na ushauri huo ukafanyiwe kazi..
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.