Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Namtumbo wametakiwa Kuimarisha Ulinzi katika Maeneo ya Hifadhi ili kulinda rasilimali za Misitu.
Agizo hilo limetolewa leo na Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Ngollo Malenya baada ya kufanya Ukaguzi wa Hifadhi ya msitu wa Matogoro B upande kijiji cha Luhimbalilo katika kata ya Mputa. Ngollo Malenya amewataka Wananchi katika kijiji hicho Kuondoka haraka katika Maeneo na kuendelea kulinda na kutunza mazingira.
Malenya amewaonya viongozi wa vijiji na Kata kujiepusha na utoaji wa vibali vya kuwaruhusu Wananchi kuingia na kufanya Shughuli mbalimbali za Kibinadamu ikiwemo kilimo na ufugaji katika Hifadhi hiyo.
"Sisi kama Kamati ya Ulinzi na Usalama tutaendelea kufuatilia na kuhakikisha kwamba Uharibifu haufanyiki kwa ajili ya Maslahi ya Wana Namtumbo n Mkoa wa Ruvuma kwa Ujumla"- Amesema Malenya.
Meneja Uhifadhi wa Misitu Tanzania katika Wilaya ya Namtumbo Vicent Walter amekili kupokea maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya na Kuyatendea kazi ikiwemo kuongeza Doria katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika Hifadhi hiyo ya Matogoro B.
Hifadhi ya Matogoro B ina ukubwa wa Hekta Elfu Thelathini na Mbili na Miatisa 32,900 ambayo inapatikana katika Tarafa ya Undendeule katika kata 5 za Mputa,Mgombasi,Litola,Namtumbo na Hanga
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.