Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo (CMT) imetembelea Ujenzi wa Mradi wa Shule ya Sekondari ya Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyopo Katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma.
Katika Ziara hiyo iliyo ongozwa na Eprehem Kawonga akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Ndg. Philemon Mwita Magesa wametembelea Ujenzi wa Madarasa 22, Maabara 4, Jengo moja la Tehama, Jengo la Maktaba , Ofisi 7 za walimu,Nyumba 5 za Walimu,Mabweni 9 na Bwalo kubwa la kisasa na ukumbi wa Kulia Chakula.
Kawonga amewataka Wakandarasi na Mafundi kufanya kazi kwa Ubora kwa kuzingatia Viwango halisi vilivyowekwa na Ofisi ya Rais Tamisemi.
"naombeni mafundi na wakandarasi fanyeni kazi kwa kuzingatia Ubora ulio kusudiwa na serikali yetu, Pia ongezeni kasi ya Ujenzi ili Miundombinu hii iweze kutumika kwa wakati na wanafunzi wetu tukiona Mnasuasua katika utekelezaji wa Miradi tutavunja mikataba yenu Fanyeni kazi kwa Kwa Viwango Sahihi", amesema Kawonga.
Kawonga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutenga Fedha nyingi kwaajili ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo kujenga Shule hiyo kubwa ya kisasa ya Wasichana (Shule ya Sekondari ya Wasichana Dkt. Samia Suluhu Hassan) ambayo inafundisha masomo ya Sayansi Pekee yenye uwezo wa kuchukua Wanafunzi Zaidi ya 1,500 kuanzia kidato cha Kwanza Hadi kidato cha Sita.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.