WAFANYABIASHARA WADOGO LITOLA WALIA NA MIKOPO KAUSHA DAMU..
Wafanyabiashara wadogo katika Kijiji Cha Litola Wilayani
Namtumbo Mkoani Ruvuma walalamikia mikopo kutoka kwenye Taasisi zisizorasmi kuwakopesha pesa Kwa ajili ya kuendeshea biashara zao Bila kupata faida
Halima Thabiti mkazi wa Kijiji Cha Litola alisema Kuna watu binafsi hukopesha fedha na marejesho ya fedha hizo zinakuwa na riba kubwa kiasi ambacho hakiwapi faida zaidi ya kumnufaisha mwenye fedha.
Thabiti alidai wakopeshaji wanakopesha shilingi 100,000 na ndani ya wiki nne unarejesha shilingi 136,000 ambapo Kila jumamosi unatakiwa kutoa rejesho shilingi 34,000 na wanaposhindwa kurejesha 34,000 inapigwa riba Hali inayowaumiza Kwa kiasi kikubwa wafanyabiashara hao.
Hata hivyo Thabiti alifafanua kuwa wafanya biashara hao wanajitahidi kufanyabiashara lakini kilichopo wanawanufaisha wakopeshaji na wao kuambulia kufanyabiashara Bila kubakiwa na chochote zaidi ya kuwanufaisha wakopeshaji fedha.
Benard Sanga Mwalimu wa Shule ya Msingi Litola alisema Kijiji Cha Litola akina mama wafanyabiashara ndogondogo wapo wengi Sana Lakini sehemu kubwa ya wafanyabiashara hao hawana mitaji ya kuendeshea biashara hizo na badala yake hutegemea wakopeshaji fedha ambao nao.hutumia fursa hiyo kuwakopesha fedha Kwa riba kubwa na kufaidika kupitia akina mama hao.
Sanga Pamoja na mambo mengine alisema akina mama hao ni waaminifu katika ulipaji wa mikopo , Licha ya kuwatesa na kuwaumiza lakini wanajitahidi kufanya biashara mchana kutwa na wakati mwingine wanaposhindwa kurejesha madeni huhangaika kweli kweli ili arejeshe aendelee na biashara yake ambayo ameizoea alisema Sanga.
Amina Ngonyani Kwa upande wake aliisema yeye na wenzake walipata mikopo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Hali iliyowapa utulivu katika biashara zao .
Ngonyani aliiomba serikali kuendelea kuwakopesha wafanyabiashara hao ili waweze kufanyabiashara Kwa utulivu badala ya kukopa mikopo kausha damu kutoka Taasisi za kifedha zisizorasmi.
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.