WAKULIMA NAMTUMBO WAPATIWA MAFUNZO YA SUMUKUVU
Wakulima wa vijiji kumi katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma wamepatiwa mafunzo ya Kudhibiti sumukuvu kuanzia hatua ya uandaaji shamba, ulimaji,utiaji mbolea na hatua za kufuata katika uvunaji.
Akiongea na wakulima wa wilaya ya Namtumbo Dafrosa Jerome Afisa kilimo kutoka wizara ya kilimo aliwaambia wakulima hao kuwa moja ya njia ya kudhibiti Sumukuvu ni kufuata hatua za kilimo bora pamoja na kutumia dawa ya kuua wadudu wanaosababisha sumukuvu.(aflasafe)
Dafrosa pamoja na mambo mengine aliwafundisha wakulima hao Kwa vitendo namna ya kulima,kupanda ,utiaji wa mbolea , utiaji dawa ya kuua wadudu wanaosababisha Sumukuvu pamoja na hatua za uvunaji Ili kuwakwepa wadudu wanaosababisha Sumukuvu kutoingia katika mazao ya mkulima.
Michael Gambi afisa kilimo wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo ambaye pia ni mratibu wa kudhibiti sumu kuvu katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo alitaja vijiji ambavyo vikundi vyake vimepatiwa mafunzo hayo ni Utwango,Msindo,Nahoro,Mawa,na Luhimbalilo.
Gambi Alivitaja vijiji vingine ambavyo vimepatiwa mafunzo hayo kuwa ni Naikesi,Nangero,Mfuate -likuyu, Namtumbo pamoja na Minazini vyote vya wilaya hiyo ya Namtumbo.
Pamoja na hayo Gambi alidai mafunzo hayo yaliambatana na ugawaji wa mbegu za mahindi aina ya ASA T105 Kwa wakulima 30 Kwa Kila Kijiji ,mbolea ya kupandia aina ya DAP Kwa mashamba darasa ,kamba ,pamoja na kiatilifu (Atlasafe) kuuua wadudu wanaosababisha Sumukuvu kwenye mazao.
Naimu Saweji Luambano mkazi wa Kijiji Cha Nangero wilayani Namtumbo alidai mafunzo hayo yamewasaidia w inakulima kujua kanuni Bora za kilimo lakini pia kujua namna ya kudhibiti mazao yasiathirike na sumukuvu kuanzia hatua ya kuandaa shamba mpaka kuvuna .
Luambano alifafanua kuwa wakulima wamefundishwa kutenganisha mahindi mabovu na mazuri Ili kuepuka sumukuvu katika mazao Ili kuepukana na homa zitokanazo na kula vyakula zilizokuwa na sumukuvu.
Pamoja na kuishukuru Serikali kuwaletea wakulima hao mafunzo. Luambano aliiomba Serikali kuendelea Kutoa elimu hiyo Kwa wakulima wengi na katika vijiji vyote vya wilaya ya Namtumbo tofauti na ilivyo hivi Sasa ambapo ni vijiji vichache ndivyo vimepatiwa mafunzo hayo.
Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Ina jumla ya vijiji 66 na mamlaka ya miji midogo miwili na kati ya vijiji hivyo vijiji 10 vimepatiwa mafunzo ya Sumu kuvu.
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.