Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametenga Fedha nyingi kwaajili ya Utekelezaji wa Ujenzi wa Miundombinu ya Shule na Matundu ya Vyoo katika Shule za Sekondari na Msingi kupitia mpango wa BOOST na SEQUIP katika Wilaya ya Namtumbo.
Hata hivyo Walimu wa Shule za Sekondari na Msingi ambapo Miradi ya BOOST na SEQUIP inaenda kutekelezwa wamepata Mafunzo maalum ili kufanya Tasmini na Majaribio ya Mfumo wa NEsT, Semina hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo imehudhuliwa na Walimu wenye Miradi hiyo,Mhandisi wa Wilaya ya Namtumbo,Maafisa Mipango, Afisa Manunuzi Wilaya na Wasaidizi, Afisa wa Teknolojia, Habari na Mawasiliano na Maafisa Elimu (msingi na sekondari) Kujifunza namna ya kutumia Mfumo Mpya wa Manunuzi wa NEsT.
Hata hivyo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Nanungu amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mifumo Bora na Rafiki ya Manunuzi ili kuhakikisha Manunuzi ya Mahitaji ya Umma yanafanyika kwa Haki na kwa Uwazi.
Vilevile Semina hii ya kuhusu Mfumo wa Manunuzi NEsT itaendelea kutolewa katika Idara Mbalimbali ikiwemo Afya na Idara zingine katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.