MIKAKATI IONGEZWE YA KUWATAKA WANANCHI WAPIME VVU KWA HIARI.
Katibu tawala wa wilaya ya Namtumbo Aden Nchimbi alimwakilisha mKuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme katika maadhimisho ya Siku ya ukimwi duniani ambapo kimkoa yalifanyika uwanja wa taifa wilaya ya Namtumbo .
Katika hotuba yake kwa wananchi amewataka kuongeza jitihada za kuwa na mazoea ya kupima virusi vya ukimwi mara kwa mara ili kuishi maisha yenye faraja pale unapogundulika kuatdhirika na virusi hivyo kwa kuanza kupata dawa mapema na kuijiongezea muda wa kuishi na wale ambao watabainika kuwa salama wachukue tahadhari na kubadili mienendo ya maisha yao ili wasiambukizwe
Pia Nchimbi alitoa wito kwa taasisi na mashirika yanayotoa huduma za upimaji wa virusi vya ukimwi kwa wananchi kuongeza mikakati ya kuwataka wananchi waweze kujitokeza kwa wingi kupima virusi vya ukimwi kwa hiari yao.
Jairy Khanga mganga mkuu wa Mkoa wa Ruvuma katika taarifa yake ailidai mkoa wa Ruvuma unavituo vya kutolea huduma za afya 348 ambapo vituo 295 sawa na asilimia 85 vinatoa huduma ya unasihi na upimaji ,289 sawa na asilimia 83 vinatoa huduma ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama wajawazito na wanaonyonyesha kwenda kwa mtoto.vituo 165 sawa na asilimia 47 vinatoa huduma ya tiba na matunzo ya watu wanaoishi na virusi vya ukumwi , vituo 41 sawa na asilimia 12 vinatoa huduma za tiba kinga vya virusi vya ukimwi kabla ya kudhurika na vituo 30 sawa na asilimia 9 vinatoa huduma za tohara kwa wanaume.
Hata hivyo bwana Khanga alisema mkoa wa Ruvuma upo juu kimaambukizi zaidi ya kiwango cha taifa cha maambukizi kwa asilimia 0.9 kadiri ya matokeo ya utafiti wa kiashiria cha UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016mpaka 2017.
Bwana Khanga alisema licha ya kiwango cha maambukizi kimkoa kuwa asilimia 5.6 na kukizidi kiwango cha maambukizi kitaifa ambacho ni asilimia 4.7 mkoa huo umepunguza ongezeko la maambukizi kutoka asilimia 7 mwaka 2011-2012 mpaka kufikia asilimia 5.6 sawa na asilimia 1.4 hivi sasa.
Mohamedi Ally Geho katibu wa baraza la watu wanaoishi na virusi vya ukimwi katika wilaya ya Namtumbo aliwataka wananchi wenzake kujitokeza kupima virusi vya ukimwi na kupata huduma za afya ili kuishi kwa matumaini kwa kuwa yeye anaendelea kuishi na sasa anazaidi ya miaka 16 tangu agundulike anavirusi vya ukimwi
Naye Rabia Miraji Gunda kutoka kijiji cha Suruti aliwaambia wananchi katika maadhimisho hayo kuwa yeye aligundulika na virusi vya ukimwi wakati wa ujauzito wake na hivyo amejifungua mtoto na kupatiwa huduma za kiafya yeye pamoja na mtoto wake hali zao zinaridhisha na hawana wasiwasi wowote.
Maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 1mwezi Desema ambapo kwa mwaka huu 2020 kauli mbiu ya Maadhimisho hayo ilikuwa “Ushirikiano wa Kimataifa ,Uwajibikaji wa pamoja”
MWISHO.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: S.L.P 55 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0765142640
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2018Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.