DC NAMTUMBO AKAGUA MIRADI YA UJENZI
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Ngollo Malenya amefanya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa madarasa ,vyoo, chumba Cha kujifungulia na Kutoa maagizo mbalimbali.
Malenya alianza ziara ya kukagua chumba Cha kujifungulia katika zahanati ya Kijiji Cha Lumecha ,Shule shikizi ya Lumecha ,shule ya Sekondari Namabengo, Shule mpya ya Suruti pamoja na Shule ya msingi Namwaya.
Katika ukaguzi huo Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Ngollo Malenya alisisitiza uwajibikaji wa kamati katika kusimamia ujenzi Kwa kuhakikisha mafundi wanalipwa stahili zao , vifaa vinanunuliwa Kwa wakati na mafundi wafanye kazi ya ujenzi na kukamilisha miradi Kwa wakati alisisitiza Malenya.
Ziara ya mkuu wa wilaya ya Namtumbo Ngollo Malenya ya kukagua miradi ya ujenzi katika wilaya ya Namtumbo
inaendelea Kwa siku ya pili huku akiwasisitiza wasimamizi wa miradi hiyo pamoja na mambo mengine kuzingatia miongozo katika usimamizi na ujenzi wa miradi hiyo iliyowekwa na Serikali..
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.