DC NAMTUMBO ACHANGIA BATI 75 UJENZI WA NYUMBA YA MTUMISHI U.W.T.
MKuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Dkt Julius Kenneth Ningu amechangia bati 75 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa umoja wa wanawake wa Chama Cha mapinduzi wilaya ya Namtumbo .
Akiongea wakati wa kukabidhi bati hizo mkuu wa wilaya ya Namtumbo Dkt Ningu aliwaambia viongozi wa umoja huo kuwa ameguswa na jitihada inayofanywa na umoja huo wa kujenga nyumba ya mtumishi wao hali iliyomfanya naye achangie bati 75 ili kuwatia moyo na kuwaongezea ari ya kujituma Zaidi ili waweze kufanikiwa lengo walilojiwekea .
Aden Nchimbi Katibu tawala wa wilaya ya Namtumbo alisema bati hizo zilinunuliwa kwa shilingi 2,625,000 ambapo kila bati lilinunuliwa kwa shilingi 35,000 kila moja na kukabidhiwa uongozi wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi wilaya ya Namtumbo.
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi wilaya ya Namtumbo Nuru Ndimbo pamoja na kumshukuru Mkuu wa wilaya ya Namtumbo kwa kuchangia bati 75 ,alisema Mkuu wa wilaya huyo ni msaada mkubwa kwa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi lakini pia kwa wananchi wote wa wilaya ya Namtumbo kwa kusimamia shughuli za maendeleo ya jamii.
Aidha Katibu wa umoja huo Elifuraha Sumary alidai umoja wa wanawake wilaya ya Namtumbo wanajivunia kuwa na mkuu wa wilaya huyo kwa madai kuwa mchango wake wa fedha,mawazo ya uhamasishaji wa ujenzi huo ndio tegemeo la umoja huo toka walipopitisha wazo la kujenga nyumba ya mtumishi wao mkuu wa wilaya huyo yupo nao na hata kufikia kuchangia bati 75 za kuezekea jengo la mtumishi wao alisema katibu.
Kwa Mujibu wa Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi Shaibu Majiwa alisema ujenzi wa Nyumba ya Mtumishi wa Umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi wilaya ya Namtumbo unafanyika katika kiwanja kilichopakana na eneo la jumuiya ya Mbarangāandu na eneo la shule ya sekondari ya Nasuli jiraji kabisa na kiwanja cha mpira wa shule hiyo.
Majiwa alifafanua kuwa ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi wilaya ya Namtumbo ulianza kujengwa .mwaka 2021 kwa kutegemea michango kutoka kwa wanachama wa umoja huo pamoja na wadau mbalimbali.
NA Yeremias Ngerangera
NAMTUMBO.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
HakimilikiĀ©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.