DIWANI AWATAKA VIONGOZI WA SERIKALI KUWAJENGA WANANCHI KISAIKOLOJIA MIGOGORO YA WANYAMAPORI NA BINADAMU
Diwani wa kata ya Likuyu Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma Kassimu Gunda aliwataka viongozi wa Serikali Kuwajenga wananchi kisaikolojia hasa kwenye migogoro kati ya binadamu na wanyamapori.
Gunda alisema ipo Tabia ya viongozi kutojitokeza kwenye migogoro kati ya wanyamapori na binadamu hasa linapotokea binadamu kuuawa na Tembo Kwa kuogopa Wananchi kuwa na hasira Kwa viongozi wao badala ya viongozi kuungana na wananchi Kuwajenga kisaikolojia ili wajue viongozi wao nao wanaumia na matatizo wanayowapata wananchi wao.
Gunda alifafanua faida ya viongozi kuwa na wananchi wakati wa matatizo Yao unawajenga wananchi kisaikolojia kuwa unajali matatizo Yao Kwa kushirikiana nao bega Kwa bega .
Hata hivyo Gunda alidai uwepo wa viongozi wakubwa katika migogoro ya wananchi wanakuwa na Imani na viongozi wao pale wanapoona wanajitokeza katika shida zao na kuwapa pole na faraja .
Pamoja na hayo yote Gunda aliiomba serikali Kuharakisha kifutajasho ili wananchi walioathirika na uharibifu wa mazao Yao na wanyamapori waweze Kununua chakula ambacho kiliharibiwa na wanyamapori hao.
Menas Fusi mkazi wa kitongoji Cha mfuate Kijiji Cha Likuyu alisema kasi ya wanyama Tembo Kuja katika mashamba ya wakulima imepungua Kutokana na kuwepo Kwa Jeshi la TANAPA ambalo Kwa kiasi kikubwa hufanya kazi ya kuwarudisha Tembo hao katika hifadhi .
Fusi alisema Tembo mmoja mwenye mtoto alimsababishia kifo Merania Lukas Magazini (62) mkazi wa Kijiji Cha Likuyu aliyekuwa amejihimu shambani na alipofika maeneo ya msituni akakutana na Tembo huyo na kumsababishia kifo.
Hata hivyo Fusi aliiomba serikali kufanya utafiti wa Tembo waliovuka mipaka Yao Kwa kuwa sio wengi wawarudishe kwenye hifadhi ya wanyama badala ya kuwaacha katika misitu ya vijiji .
Afisa Maliasili na Utalii wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo priska Msuha alisema Licha ya kutokea Changamoto ya Tembo mmoja mwenye mtoto kumua mwananchi katika Kijiji Cha Likuyu Changamoto ya Tembo imepungua Kutokana na Kambi ya TANAPA kufanya kazi kubwa ya kuwarudisha wanyamapori hao hifadhini lakini pia wananchi Kujua madhara na namna ya kukabiliana na Tembo wanapoingia katika makazi ya watu.
Priska alisema huko Nyuma kabla ya kutolewa elimu ya namna yakufanya wakimwona mnyama Tembo ,wananchi waliokuwa wakimwona Tembo katika makazi yao waliokuwa wanapiga kelele na kumfuata lakini Kwa Sasa wananchi wakimwona Tembo hawamfuati hubaki kimya hupiga simu ili mamlaka zinazohusika hufika haraka na kuwaondoa Tembo hao katika makazi ya watu.
Hata hivyo watumishi wa idara ya Maliasili na Utalii Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo wametawanywa katika maeneo yenye Changamoto ya Tembo kuingia katika makazi ya watu ili kushirikiana na askari wasaidiazi wa wanyapori wa vijiji katika kukabiliana na Changamoto zitakazojitokeza kutoka Kwa wanyama hao.
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.