Kamati ya MFUKO wa Jimbo , Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo chini ya Mwenyekiti wake MHE. VITA RASHID KAWAWA Ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Namtumbo imeidhinisha Matumizi ya Fedha za MFUKO wa Jimbo Tsh.Milioni tisini na tisa( 99,000,000 )kwaajili ya Kuchochea Utekelezaji wa MIRADI mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo Miradi ya Afya, Elimu na Miradi mbalimbali iliyoibuliwa Kwa nguvu za Wananchi.
Kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Mhe. Vita Kawawa kikiudhuliwa na Wajumbe mbalimbaliikiwemo baadhi ya wataalam wa CMT na Madiwani kutoka Katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.