MADUDU UKAGUZI MADUKA YA DAWA MUHIMU NAMTUMBO
Mganga mkuu wa wilaya ya Namtumbo Dkt.Aaron Hyera alifanya ukaguzi wa kushtukiza katika baaadhi ya maduka ya dawa muhimu na kubaini madudu kwenye maduka hayo!
Akiongea baada ya ukaguzi wa maduka mawili ya dawa muhimu katika Kijiji Cha Ligunga mamlaka ya mji mdogo wa Namtumbo alisema aliamua kufanya ukaguzi huo wa kushtukiza Ili kujionea halihalisi katika maduka hayo ya dawa muhimu na kubaini madudu katika maduka hayo.
Dkt .Aaron Hyera alikamata dawa zilizopitwa na wakati ,
lakini pia alikamata dawa ambazo haziruhusiwi kuuzwa katika maduka ya dawa muhimu na badala yake kwenye vituo vya afya na hospitali za wilaya.
Hata hivyo Dkt Hyera alibaini wauza dawa katika maduka hayo kutokuwa na vibali Vilivyowaidhinisha kuuza dawa katika maeneo ambayo hayajakaguliwa na mamlaka husika .
Dkt .Hyera aliwaambia wauza dawa muhimu kuwa dawa zao zinachukuliwa na ofisi yake mpaka watakapokidhi vigezo vya kisheria vya wao kuendelea kuuza maduka ya dawa muhimu kwa kufuata taratibu za uuzaji na umiliki wa maduka ya dawa muhimu.
Mtendaji wa mamlaka ya mji mdogo wa Lusewa Viligilia Shawa alidai wauzaji hao walikuwa wanaambiwa kufuata utaratibu wa kisheria wa uanzishaji wa maduka ya dawa na kupata leseni lakini hawakutaka kufanya hivyo mpaka ukaguzi unawakuta hawana vibali vyovyote na mbali zaidi kuuza dawa ambazo zimepitwa na wakati lakini kufanya tiba ambayo haipaswi kufanya katika maduka ya dawa muhimu .
Prosperia Maguga na ELmina Maurus Msuha wauzaji wa maduka ya dawa muhimu katika Kijiji Cha Ligunga walimwambia Mganga mkuu wa wilaya kuwa wanakubaliana na maelekezo yaliyotolewa na mganga mkuu huyo na wapo tayari kufuata utaratibu wa kisheria wa umiliki na uuzaji wa maduka ya dawa muhimu.
Husein Mkundi na Matola Mpichila wananchi wa Kijiji Cha Ligunga waliipongeza Serikali Kwa kufanya ukaguzi kwenye maduka hayo ya dawa na kubaini dawa zilizopitwa na wakati huku wananchi wakiendelea kuuziwa dawa hizo ambazo zimepitwa na wakati ambazo ni hatari Kwa afya za watumiaji.
Mkundi na Mpichila waliomba Serikali kuhakikisha zahanati za Serikali zinakuwa na dawa za kutosha badala yake ukifika kwenye zahanati za Serikali unaambiwa dawa hakuna nenda kwenye duka la dawa kanunue na ukifika kwenye duka la dawa muhimu unakutana na dawa zilizopitwa na wakati na wananchi hawajui hununua na kwenda kutumia walisema wananchi hao.
Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo inaendelea kufanya ukaguzi wa maduka ya dawa muhimu kwa kushtukiza Ili kujiridhisha na vigezo vya uanzishwaji na uuzaji vya maduka na wale wasiokidhi vigezo maduka Yao yatafungwa mpaka yatakapokidhi vigezo vya kisheria vilivyopo.
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.