MAMBO MATATU KUIBADILISHA NAMTUMBO
Na Yeremias Ngerangera....Namtumbo
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Philemon Mwita Magesa ameyasema hayo wakati akizungumza na wakuu wa idara na vitengo katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo.
Magesa ameripoti katika Halmashauri ya Namtumbo akitokea Halmashauri ya Tunduma na kudai kuwa mambo matatu yakisimamiwa Kwa nguvu zote Namtumbo itabadilika Kwa Kasi.
Alitaja mambo hayo ni Pamoja na ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri ambapo alidai wakuu wa idara na vitengo kuhakikisha Kila mtu anahusika katika ukusanyaji wa mapato ,
Jambo jingine ni kuwataka wakuu wa idara na vitengo kutenga siku mbili au tatu katika wiki kusimamia miradi ya ujenzi inayotekelezwa katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo.
Hata hivyo Magesa alidai utawala Bora ni jambo jingine muhimu wakati wa kusimamia ,kutekeleza majukumu ya kikazi katika utumishi wa umma.
Aidha Magesa alifafanua swala la ukusanyaji wa mapato kuwa ni jambo muhimu katika Halmashauri na swala Hilo halitakiwi kuachiwa watu wa idara ya fedha Bali ni jambo la Kila mkuu wa idara ,kitengo na watu wote wa wilaya ya Namtumbo alisema Magesa.
Mkuu wa idara fedha Pendo Nyomeye alisema ni kweli kabisa swala la ukusanyaji wa mapato wasiachiwe watumishi wa idara ya fedha kitengo Cha mapato pekee Bali tuongeze nguvu Kwa kushirikiana Pamoja ili kuongeza mapato ya Halmashauri ya Namtumbo.
Paul Ambokile mkuu wa idara ya mifugo na uvuvi wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo alisema kuwa watumishi wa Halmashauri hiyo wapo tayari kusimamia mambo hayo matatu ili kuweza kuibadisha Namtumbo iweze kuendelea
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.