MAMENEJA,WAHASIBU CBWSO RUVUMA WAPATIWA MAFUNZO
Mameneja na Wahasibu wa vyombo vya huduma ya watumiaji maji (CBWSO) katika Wilaya za Mkoa wa Ruvuma Walipatiwa mafunzo ya Siku 10 katika ukumbi wa Heritage uliopo Msamala Manispaa ya Songea.
Lengo la mafunzo hayo ni kuwafundisha Mameneja na Wahasibu wafahamu mabadiliko yaliyofanywa na Serikali ya kulipa bili ya maji kutoka fedha taslimu na kwenda kulipa bili Kwa kutumia mfumo wa MAJI'IS .
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Ruvuma Rebman Nganshonga aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kusimamia maagizo ya Serikali katika kutekeleza majukumu Yao kazini.
Hata hivyo Nganshonga aliwaagiza washiriki na waratibu wa Wilaya wa vyombo vya huduma ya watumia maji kusajiri wateja katika mfumo wa MAJI'IS na pia aliwataka viongozi wa CBWSO kuhakikisha akaunti zote zinafungwa Kwa kuwa akaunti ya makusanyo ni ya BOT huku akiwaeleza akaunti zitakazobaki ni akaunti za matumizi pekee.
Pamoja na hayo Nganshonga aliwaagiza viongozi hao kutunza nyaraka zote za vyombo vya watumia maji na kuanza kutumia mfumo ukusanyaji bili za maji MAJI'IS.
Mratibu wa vyombo vya watumia maji CBWSO Wilaya ya Namtumbo George Mswaya alisema anaishukuru serikali Kwa kuandaa mafunzo ili kuwawezesha mameneja na wahasibu kujengewa uwezo wa kutumia mfumo wa MAJI'IS Pamoja na kupatiwa miongozo mbalimbali itakayowaganya waweze kufanyakazi Kwa ubora Kwa Kwa ufanisi.
Ofisi ya RUWASA Mkoa wa Ruvuma Kwa kushirikiana na ofisi za RUWASA za Wilaya zitaandaa matangazo ya kutoa elimu Kwa wananchi ili wafahamu mabadiliko ya kulipa bili ya maji kutoka fedha taslimu na kwenda kutumia mfumo wa MAJI'IS ili kuwarahisishia viongozi wa vyombo vya watumia maji ambao wamepatiwa mafunzo ya kutumia mfumo huo.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.